Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 09:34

Uhispania yashinda taji la nne la ubingwa katika fainali ya Euro 2024


Mshambuliaji wa Uhispania Alvaro Morato akiwa ameshikilia kombe na kusherekea na wachezaji wenzake, Julai 14, 2024. Picha ya AFP
Mshambuliaji wa Uhispania Alvaro Morato akiwa ameshikilia kombe na kusherekea na wachezaji wenzake, Julai 14, 2024. Picha ya AFP

Uhispania Jumapili ilishinda taji la nne la ubingwa katika fainali ya michuano ya soka ya Ulaya baada ya bao la mchezaji Mikel Oyarzabal katika dakika ya 87 kunyakua ushindi wa mabao 2 kwa moja dhidi ya Uingereza.

Oyarzabal aliingia na kupiga krosi ya Marc Cucurella, wakati mchezo huo uliochezwa kwenye uwanja wa Olympia wa mjini Berlin ulionekana kuelekea kwenye muda wa ziada baada ya Uingereza kuonyesha uthabiti katika dimba hilo.

Mchezaji Cole Palmer aliyetokea benchi aliisawazishia Uingereza dakika ya 73 na kufuta bao la kwanza la mchezaji wa Uhispania Nico Williams dakika ya 47 kwa kupewa pasi na Lamine Yamal, kijana mwenye umri wa miaka 17.

Uhispania ilishnida pia taji mwaka 1964, 2008 na 2012.

Uingereza imekuwa ikishindwa mara kwa mara katika michezo ya fainali ya Ulaya na haijashinda taji lingine tangu kuwa mshindi wa kombe la dunia mwaka 1966

Forum

XS
SM
MD
LG