Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa mjini Paris ilieleza kuwa ghasia za hivi karibuni zilizuolenga ubalozi wa Ufaransa huko Niamey, mji mkuu, ni moja ya sababu ya uamuzi huo.
Kufungwa kwa anga ya Niger pia “inawaacha watu wetu hawana njia ya kuondoka nchini humo kwa kutumia usafiri wao wenyewe,” wizara hiyo ilisema.
Kuondolewa kwa raia hao kumekuja wakati mgogoro ukiongozeka uliochochewa na mapinduzi ya wiki iliyopita dhidi ya rais aliyechaguliwa kidemokrasia, Mohamed Bazoum.
Safari hiyo ya kuwaondoa ilianza Jumanne kwa raia wa Ufaransa na nchi nyingine za Ulaya ambao wanataka kuondoka Niger, wizara ya Ufaransa ilisema katika taarifa yake.
Haikutoa maelezo zaidi. Inakadiriwa kuwa mamia ya raia wa Ufaransa hivi sasa wako nchini Niger, koloni la zamani la Ufaransa.
Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AP
Forum