Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 13, 2025 Local time: 20:09

Kremlin inazitaka pande zote nchini Niger kujizuia na machafuko


Rais aliyepinduliwa nchini Niger Mohamed Bazoum akiwa mjini Niamey, Niger. March 16, 2023.
Rais aliyepinduliwa nchini Niger Mohamed Bazoum akiwa mjini Niamey, Niger. March 16, 2023.

Katika mapinduzi ya tatu baada ya miaka mingi dhidi ya kiongozi katika eneo la Sahel, mkuu wa kikosi cha ulinzi wa Rais Jenerali Abdourahamane Tiani alijitangaza kiongozi na alisema hatua hiyo ni majibu ya kudhoofika kwa hali ya usalama inayohusishwa na umwagaji damu unaofanywa na wanajihadi

Kremlin siku ya Jumatatu imezitaka pande zote nchini Niger kujizuia na machafuko ambako utawala wa kijeshi ulichukua madaraka wiki iliyopita kwa njia ya mapinduzi na walimkamata Rais Mohamed Bazoum.

"Tunatoa wito wa kurejeshwa haraka kwa utawala wa sheria nchini humo na kwa pande zote kujizuia na ghasia ili kuepuka vifo kwa binadamu", msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov alisema.

Katika mapinduzi ya tatu baada ya miaka mingi dhidi ya kiongozi katika eneo la Sahel mkuu wa kikosi chenye nguvu cha ulinzi wa rais Jenerali Abdourahamane Tiani alijitangaza kiongozi. Tiani alisema hatua hiyo ni majibu ya kudhoofika kwa hali ya usalama inayohusishwa na umwagaji damu unaofanywa na wanajihadi, rushwa, pamoja na matatizo ya kiuchumi.

Viongozi wa kiafrika siku ya Jumapili waliipa serikali ya kijeshi wiki moja ya kurejesha madaraka au kukabiliana na uwezekano wa matumizi ya nguvu. Kinachofanyika nchini Niger ni suala linaloleta wasiwasi mkubwa, Peskov alisema.

Bazoum ni mmoja katika kundi linalopungua idadi ya marais waliochaguliwa na wanaounga mkono mataifa ya magharibi katika ukanda wa Sahel ambako tangu mwaka 2020 uasi wa kijihadi pia umechochea mapinduzi nchini Mali na Burkina Faso.

Mivutano ilikuwa juu siku ya Jumatatu wakati utawala mpya wa kijeshi umeushutumu utawala wa zamani wa kikoloni Ufaransa kwa kutaka kuingilia kati kijeshi ili kumrejesha madarakani Bazoum.

Forum

XS
SM
MD
LG