Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 06, 2024 Local time: 21:18

Uchaguzi wa rais wafanyika Tunisia


Mgombea urais wa Tunisia Zouhair Maghzaoui (kulia) apiga kura katika kituo kimoja mjini Tunis, Tunisia (Oktoba 6, 2024). Pivca na REUTERS/Zoubeir Souissi
Mgombea urais wa Tunisia Zouhair Maghzaoui (kulia) apiga kura katika kituo kimoja mjini Tunis, Tunisia (Oktoba 6, 2024). Pivca na REUTERS/Zoubeir Souissi

Raia wa Tunisia walipiga kura siku ya Jumapili katika uchaguzi wa rais, huku mgombea aliye madarakani Kais Saied akitarajiwa kupata miaka mingine mitano madarakani wakati wakosoaji wake wakuu wakiwa gerezani.

Miaka mitatu baada ya Saied kuingia madarakani, uchaguzi huo unaonekana kama hatua ya mwisho katika majaribio ya demokrasia ya Tunisia. Nchi hiyo ya Afrika Kaskazini ilikuwa imejivunia kwa zaidi ya muongo mmoja kwa kuwa chimbuko la mageuzi maarufu kama Arab Spring dhidi ya udikteta.

Bodi ya uchaguzi ya ISIE ilisema takriban watu milioni 9.7 walitarajiwa kujitokeza. Takriban 47% yao wana umri wa kati ya miaka 36 na 60. Katika kituo kimoja cha kupigia kura katikati mwa Tunis, kundi la wanaume wengi wazee walionekana wakipanga foleni kupiga kura.

"Nilikuja kumuunga mkono Kais Saied," Nouri Masmoudi mwenye umri wa miaka 69 alisema. "Familia yangu yote itampigia kura." Fadhila, mwenye umri wa miaka 66, alisema alipiga kura "kujibu wale waliotoa wito wa kususia zoezi hilo."

Kituo kilikuwa kimeshuhudia "mmiminiko mzuri wa wapiga kura," wengi wao wakiwa zaidi ya umri wa miaka 40, mkurugenzi wake, Noureddine Jouini, alisema, huku kukiwa na wapiga kura 200 katika nusu saa ya kwanza ya upigaji kura.

Saa moja baada ya kupiga kura, Farouk Bouasker, mkuu wa ISIE, alisema bodi hiyo ilishuhudia "idadi kubwa" ya wapiga kura. Katika kituo kingine katika mji mkuu, Hosni Abidi, 40, alisema anahofia udanganyifu katika uchaguzi.

Forum

XS
SM
MD
LG