Takriban raia 12 wa Tunisia wakiwemo watoto watatu wagundulika wamekufa baada ya boti ya wahamiaji kupinduka kwenye pwani ya kisiwa cha kusini mashariki cha Djerba leo Jumatatu, afisa wa mahakama amesema.
Boti ilizama nyakati za aflajiri na watu 29 wameokolewa, msemaji wa Medenine, Fethi Baccouche ameliambia shirika la habari AFP, akiongezea kuwa wanaume watano na wanawake wanne ni miongoni mwa waliokufa, na kuwa sababu ya boti kuzama haijulikani.
Kikosi cha ulinzi wa pwani cha Tunisia kimesema kilipokea tahadhari kutoka kwa wahamiaji wanne ambao waliogelea hadi ufukweni. Tunisia na nchi jirani ya Libya zimekuwa ni vituo vikuu vya wahamiaji kuanzia safari zao wakitafuta maisha bora Ulaya, mara nyingi wakijitia katika hatari kubwa wanapovuka bahari ya Mediterranean.
Mmiminiko wa wahamiaji umechochewa na uchumi usiokuwa wa Tunisia, huku asilimia 0.4 ya ukuaji ulishuhudiwa mwaka 2023 na kiwango cha ukosefu wa ajira kilipanda sana. Nchi hiyo ya Afrika Kaskazini pia imetikishwa na mivutano ya kisiasa, baada ya Rais Kais Saied kufanya mabadiliko ya kujilimbikizia madaraka Julai 2021.
Kila mwaka, maelfu ya watu wanajaribu kufanya safari kwenda Italy, katika kisiwa cha Lampedusa kilichopo kiasi cha kilometa 150, ikiwa ndiyo bandari yao ya kwanza.
Forum