Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 03, 2025 Local time: 07:35

Uchaguzi wa Bunge na Mitaa wa Belarus wafanyika, licha ya Upinzani kuomba ususiwe


Waandamanaji dhidi ya Rais wa Belarus nje ya bunge la EU, mjini Brussels.
Waandamanaji dhidi ya Rais wa Belarus nje ya bunge la EU, mjini Brussels.

Uchaguzi wa bunge na mitaa nchini Belarus umefanyika Jumapili, licha ya wito wa kuususia kutoka kwa upinzani, ukitarajiwa kuimarisha utawala wa kimabavu wa rais Alexander Lukashenko, ambaye ameongoza taifa hilo kwa karibu miaka 30.

Lukashenko amedai kuwa mataifa ya magharibi yanajaribu kutumia kura hiyo kuhujumu serikali yake, pamoja na kuyumbisha taifa hilo lenye wakazi milioni 9.5. Wengi wa wagombea walioshiriki uchaguzi huo ni kutoka vyama 4 vilivyosajiliwa vya Beyala Rus, Communist, Liberal na kile cha Labor and Justice.

Vyama vyote hivyo vinaunga mkono sera za Lukashenko, wakati takriban vyama nusu darzeni vikiwa vimenyimwa usajili. Kiongozi wa upinzani Sviatlana Tsihanouskaya, ambaye anaishi uhamishoni kwenye nchi jirani ya Lithuania baada ya kugombea urais dhidi ya Lukashenko 2020, alitoa wito kwa wapiga kura kususia zoezi hilo.

Uchaguzi wa Jumapili ni wa kwanza tangu ule wa 2020 wenye utata, na ambao ulitoa muhula wa 6 kwa Lukashenko, na kupelekea maandamano makali kote nchini humo, yakipelekea kukamatwa kwa zaidi ya watu 35,000. Baadhi ya vyombo vya habari vilipigwa maraufuku, huku mashirika yasio ya kiserikali yakifungwa.

Forum

XS
SM
MD
LG