Timu hiyo ya Algeria ilikuwa haijapoteza mchezo katika mechi zake 35 zilizopita na hivyo sasa wanahitaji lazima washinde katika mchezo wao wa mwisho dhidi ya Ivory Coast kujihakikishia kuendelea na michuano hiyo, baada ya kutoka sare katika mechi yao ya kwanza dhidi ya Sierra Leonne.
Mchezaji wa Algeria Amir Selmane Rami Bensebaini anayecheza soka la kulipwa katika klabu ya Borussia huko Ujerumani alipiga mpira wa adhabu juu ya lango la Equatorial Guinea zikisalia dakika kumi kabla ya mpira kumalizika walipokuwa wakishambulia kwa kasi kutafuta bao la kusawazisha.
Kwa maana hii kundi hii mabingwa watetezi wanashika mkia katika kundi E huku vinara Ivory Coast wakiongoza kundi hilo kwa hiyo mechi yao ya mwisho itakuwa kali na inayosubiriwa kwa hamu.
Wakati huo huo timu ya Tunisia- Carthage Eagles walifufua matumaini yao ya kufuzu katika Kundi F kwa kuwalaza Mauritania – Mourabitounes kwa mabao 4-0 mjini Limbe .
Tunisia walitawala mchezo huo wakiongozwa na Wahbi Khazri ambaye alionyesha mchezo mzuri na kufunga mabao mawili kunako dakika za 8 na 64.
Mabao mengine yalifungwa na Hamza Mathlouthi katika dakika ya 4 na Seiffeldine Jaziri katika dakika ya 66.