Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Novemba 25, 2024 Local time: 09:31

Morocco yakata tiketi kuingia 16 bora


Mashabiki wa timu ya Comoros kabla ya kuanza mechi kati ya Morocco na Comoros.
Mashabiki wa timu ya Comoros kabla ya kuanza mechi kati ya Morocco na Comoros.

Timu ya taifa ya Morocco Atlas Lions imekata tiketi ya kuingia katika raundi ya pili ya michuano ya kombe la mataifa ya Afrika baada ya kuwabwaga Comoro kwa bao 2-0.

Mtanange huo wa kundi C katika uwanja wa Ahmadou Ahidjo uliwakutanisha vigogo wa soka Afrika na wawakilishi wa Afrika Mashariki wanaoshiriki kwa mara ya kwanza katika mchuano huo.

Alikuwa ni kiungo mshambuliaji Selim Amallah anayecheza ligi daraja la kwanza Ubelgiji katika timu yaStandard Liège aliyeipatia Morocco bao la kwanza kunako dakika ya 16.

Comoro walijitahidi kupambana na kuzuia mashambulizi mengi ya Morocco huku golikipa Ben Boina akifanya kazi ya ziada kuokoa hatari langoni mwake ikiwa ni pamoja na penalti katika dakika ya 83 ya mchezo iliyopigwa na En-Nesyri. Penalti hiyo ilitolewa kwa Morocco baada ya golikipa huyo kugongana na mshambuliaji Fayçal Fajr.

Mchezaji wa Morocco Sofyan Amrabat, kushoto, akimzuia mchezaji wa Comoros El Fardou Ben Nabouhane.
Mchezaji wa Morocco Sofyan Amrabat, kushoto, akimzuia mchezaji wa Comoros El Fardou Ben Nabouhane.

Morocco walifanikisha kujihakikishia kuingia raundi ya pili baada ya kupachika bao la pili lililofungwa na Zakaria Aboukhlal katika dakika ya 88 na hilo pia kupelekea mwisho wa safari ya Comoro katika michuano hiyo.

Nayo timu ya taifa ya Malawi imejiweka katika nafasi nzuri kwenye michuano hiyo baada ya kupata ushindi muhimu dhidi ya wapinzani wao wa COSAFA Zimbawe wa mabao 2-1 katika uwanja wa Stade Omnisports de Bafoussam.

Alikuwa ni mshambuliaji Gabadinho Mhango aliyepachika mabao yote mawili wakati Malawi ilipotoka nyuma na kuwashinda Wazimbabwe katika mchezo mkali na wa kusisimua Ijumaa,

Timu zote mbili zilikamiana na kushambuliana kwa zamu katika dakika za mwanzo za mchezo huo.

Zimbabwe walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Ishmael Wadi lakini Malawi walijibu mapigo na kusawazisha kabla ya mapumziko,

Kipindi cha pili kilianza kama cha kwanza kwa mashambulizi makali sana kila upande. Na hatimaye Malawi walifanikiwa kupata bao la pili na la ushindi kwa mara nyingine tena kupitia kwa Gabadinho Mhango katika dakika ya 58.

Malawi sasa wana pointi tatu kabla ya mechi yao ya mwisho ya kundi B dhidi ya Senegal siku ya Jumanne mjini Bafoussam. Zimbabwe ambayo imekwishatolewa itakamilisha ratiba kwa kupambana na Guinea mjini Yaounde.

Wakati huo huo mpambano uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu wa wababe wa soka Afrika Magharibi Lions of Teranga Senegal na Guinea wa kundi B ulimalizika kwa sare ya bila kwa bila katika uwanja wa Stade Omnisports de Bafoussam Ijumaa.

Mtanange huo uliwakutanisha nyota wawili wa Liverpool waliokuwa katika timu tofauti Sadio Mane -Senegal na Nabby Keita -Liverpool huku kila mmoja akiwa nahodha wa timu yake.

Timu hizo zilishambuliana kwa zamu na hatimaye timu zote mbili hazikuweza kupata nafasi ya kupata bao na ili kufuzu katika hatua ya 16 borazitalazimika kusubiri mechi zao za mwisho siku ya Jumanne.

Senegal itasalia Bafoussam ambako itacheza na timu ya Malawi ambapo wote wanahitaji ushindi ili kusonga mbele.

XS
SM
MD
LG