Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 17:41

Cameroon yasonga mbele katika raundi ya 16

Mshambuliaji wa Cameroon Vincent Aboubakar (Kulia) akishangilia kuifungia timu yake bao la tatu wakati wa mechi ya Kundi A ya Kombe la Mataifa ya Afrika kati ya Cameroon na Ethiopia katika uwanja wa Stade d'Olembé mjini Yaounde Januari 13, 2022. (Picha KENZO TRIBOUILLARD / AFP.

Timu ya taifa ya Cameroon imekuwa ya kwanza kutinga hatua ya mtoano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kufuatia kuwapa kichapo chao cha mabao  4-1 timu ya taifa ya Ethiopia Walya Antilopes kwenye Uwanja wa Olembe mjini Yaounde.

Timu ya taifa ya Cameroon Indomitable Lions imekuwa ya kwanza kutinga hatua ya mtoano ya Kombe la Mataifa ya Afrika la TotalEnergies 2021 kufuatia kuwapa kichapo chao cha mabao 4-1 timu ya taifa ya Ethiopia -Walya Antilopes kwenye Uwanja wa Olembe mjini Yaounde.

Nahodha Vincent Aboubakar na mwenzake Toko Ekambi walifunga mabao mawili kila mmoja baada ya Dawa Dukele kuipatia Ethiopia bao la kuongoza.

Cameroon walifikisha pointi sita na kujihakikishia nafasi ya kuingia 16 bora, huku Ethiopia wakiwa hawana pointi baada ya michezo miwili.

Waliya Antelopes walikuwa wa kwanza kupata bao ndani ya dakika nne kupitia kwa Dawa Dukele .

Kama katika mechi yao ya ufunguzi Cameroon walitoka nyuma na kushinda wakati huu kupitia kwa Karl Ekambi aliyeunganisha kwa kichwa krosi nzuri ya Collins Fai.

The Indomitable Lions sasa wamepata ushindi mfululizo kabla ya mechi yao ya mwisho ya Kundi A dhidi ya Cape Verde.

XS
SM
MD
LG