Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 12:44

Trump atoa wito Wamarekani waungane


Rais Trump akiwasili katika ukumbi wa Bunge la Congress kutoa hotuba yake ya Hali ya Taifa
Rais Trump akiwasili katika ukumbi wa Bunge la Congress kutoa hotuba yake ya Hali ya Taifa

Rais Donald Trump ametoa wito kwa Wamerekani kuungana na pia amenadi kile anachoona ni mafanikio ya sera ya nje na hali ya uchumi, katika hotuba yake ya kwanza ya Hali ya Taifa Jumanne.

“Usiku wa leo, nawaomba nyote kuweka tofauti zenu pembeni, kushirikiana katika mambo ya umoja wetu na kutekeleza umoja ambao tunatakiwa kuusimamia kwa ajili ya watu ambao walituchagua ili tuwatumikie,” amesema Trump.

Wakati wa hotuba yake iliodumu kwa dakika 80, Trump alitoa wito kwa wabunge kupitisha pendekezo lake la kubadilisha mfumo wa uhamiaji nchini na kukarabati miundo mbinu iliyoko nchini.

Kwa upande wa sera ya mambo ya nje, Trump aliahidi kuchukua msimamo mkali, na kusema kuwa atafanya bidii kuondoa “makosa ya msingi” yaliyofanyika katika makubaliano ya nyuklia ya Iran na kuonyesha “ msimamo kamili wa Marekani katika kukabiliana na suala la Korea Kaskazini.

“Uzoefu wa siku za nyuma unatufundisha kuwa kujibweteka na kulegeza masharti ndio kunakoleta uvunjifu wa amani na uchochezi. Sitorudia makosa yaliyofanywa na uongozi uliotangulia ambao umetufikisha katika hali hii ya hatari,” Trump amesema.

“Alikuwa anajaribu kutoa picha ya jinsi mwaka wake wa kwanza madarakani ulivyokuwa na mafanikio,” amesema Steven Pifer, mtafiti wa ngazi ya juu anayezuru taasisi ya utafiti ya Brookings Institution.

“Alidai utawala wake umepata mafanikio makubwa katika kuboresha uchumi kufikia hali nzuri. Baadhi ya sifa za mafanikio hayo, bila ya shaka, inarudi kwa Rais Obama, ambaye alimtangulia katika urais. Na baadae Trump aliorodhesha ajenda yake, japokuwa hakutoa maelezo kamili.

Hotuba yake ilikuwa imekosa vibwagizo vyake vya mashambulizi ambavyo Trump mara nyingi huelekeza kwa wapinzani wake. Lakini wengi wa Wademokrati katika bunge walionekana kutofurahishwa na kuzomea katikati ya maelezo kadhaa ya hotuba yake.

XS
SM
MD
LG