Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 18:47

Trump asaini makubaliano ya bajeti, aepusha serikali kufungwa


Rais Donald Trump
Rais Donald Trump

Baraza la Wawakalishi nchini Marekani limepitisha bajeti kubwa ya dola bilioni 400 baada ya kufikia makubaliano mapema Ijumaa ambayo yalikuwa na azma ya kuepukwa kufungwa kwa shughuli za serikali kuu.

Rais Donald Trump amesaini makubaliano hayo katika ikulu ya White House Ijumaa asubuhi.

Wabunge walipiga kura 240 – 186 kuidhinisha makubaliano. Hata hivyo, fedha hizo zinafadhili shughuli za serikali kuu mpaka Machi 23. Wabunge wamepewa muda wa kuandika kwa kina mpango wa matumizi kwa kipindi kilichobaki cha mwaka wa fedha ambao unamalizika Septemba 30.

Bajeti ilipitishwa, licha ya upinzani wa baadhi ya wanasiasa ambao walipinga ongezeko kubwa katika matumizi, na bila ya mpango wowote wa kuchukua hatua za kuwalinda wahamiaji vijana zaidi ya milioni moja ambao hawana makaratasi halali, wanaojulikana kama “Dreamers.”

Serikali ya Marekani ilifungwa Ijumaa asubuhi wakati bunge lililposhindwa kufikia muafaka katika muda wa mwisho ili kupitisha bajeti ya kuifadhili tena serikali kuu. Ufungaji wa baadhi ya shughuli za serikali kuu ulikuwa wa pili katika kipindi cha chini ya mwezi mmoja.

Baadaye, baraza la seneti lilipiga kura 71 – 28 kuifungua tena serikali kuu.

Seneta mmoja mrepublikan Alhamisi jioni waliitisha kikao cha pamoja kuhusu mswaada wa kuifungua serikali ya Marekani saa kadhaa kabla ya muda uliowekwa kumalizika.

Rand Paul wa jimbo la Kentucky alipinga utaratibu wa seneti wa kupigia kura makubaliano ya bajeti ya miaka miwili ambayo yataboresha matumizi ya jeshi na ya ndani kwa mabilioni ya dola, akisema huenda itasababisha kupanda kwa kiwango kikubwa nakisi ya serikali wakati ambapo Marekani tayari inakumbana na hali hiyo na kuliongezea taifa zaidi ya dola trilioni 20 ya deni la taifa.

“Siwezi, kwa kweli kabisa, na kwa nia njema kuangalia upande mwingne,” Paul amesema katika hotuba yake ndefu iliyojaa hamasa bungeni ambayo ilichukua muda mwingi ambapo bunge lingeweza kuchukua hatua kuepuka kusitisha operesheni za serikali kuu ambazo si muhimu. “Tuna mswaada wa kurasa 700 ambao hakuna ambaye ameusoma na ulichapishwa usiku.. hakuna kitakachofanyiwa mageuzi, tunaendelea kupoteza muda.”

XS
SM
MD
LG