Maoni hayo ameyatoa wakati wa hafla ya Jumanne iliowashirikisha walinzi wa usalama katika jamii za Marekani ambao wanalifuatilia genge maarufu la uhalifu la Salvatrucha maarufu kama MS-13.
Trump amerejea kugusia makosa ya jinai yanayofanywa na wahamiaji alipokuwa anasisitiza haja ya kufanyia marekebisho mpango wa uhamiaji, ambao amesema ni lazima ujumuishe kuboresha usalama wa mipakani.
Ametaka pia kusitishwa kabisa mfumo wa uhamiaji unaoruhusu familia kuleta ndugu zao na kusimamisha programu ya visa ya bahati nasibu na badala yake kuangalia taaluma ya mwombaji kama kigezo cha kupewa fursa ya kuja Marekani.
“Kama hatujabadilisha sheria, na kuondoa mianya ya kuwawezesha kuingia nchini na kuendelea kuua – wafuasi wa magenge hayo. Na tunazungumzia tu suala la MS- 13.
'Kuna wanachama wengi wa genge hilo ambao hata hawatajwi. Kama hatujabadilisha mfumo huo bora serikali ifungwe. Tutaifunga serikali,” Trump amesema.