Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 13:56

Trump anasema hatawania tena urais akishindwa kwenye uchaguzi wa Novemba 5


Donald Trump akifanya kampeni Arizona
Donald Trump akifanya kampeni Arizona

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump amesema hatawania muhula wa nne mfululizo wa urais ikiwa atashindwa kwenye uchaguzi wa tarehe 5 Novemba, akisema hayo katika mahojiano yaliyochapishwa Jumapili.

Akiulizwa ikiwa anaweza kugombea tena katika miaka minne ijayo iwapo hatafanikiwa katika kuwania kiti cha urais kwa mara ya tatu mfululizo, rais huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 78 alimwambia mwandishi wa habari wa Marekani Sharyl Attkisson: “Sidhani. Sidhani kwamba hilo litatokea. Sidhani kabisa. Tunatumai tutafanikiwa.”

Trump anakabiliwa na ushindani mkubwa dhidi ya mshindani wa chama cha Democrat Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris, huku kura ya maoni ikionyesha ushindani mkali kati ya wagombea hao wawili katika majimbo ambayo yanaamua mshindi wa uchaguzi, licha ya kuwa Harris anaonekana kuongoza katika kura ya maoni kwenye ngazi ya taifa.

Forum

XS
SM
MD
LG