Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 21:36

Trump aidhinisha mashambulizi zaidi ya angani Somalia


Rais Donald Trump
Rais Donald Trump

Wizara ya Ulinzi ya Marekani imetangaza Alhamisi kuwa Rais Donald Trump ameipa uwezo zaidi kuanzisha mashambulizi ya angani Somalia dhidi ya al-Shabab.

Wizara hiyo imesema Trump amepitisha ombi la mashambulizi yenye kulenga shabaha zaidi Somalia ili kusaidia Majeshi ya Umoja wa Afrika na Somalia yaliyoko ardhini “ kuongeza presha” kwa al-Shabab na kuwanyima fursa magaidi kugeuza Somalia kuwa mafichoni, ambako wamekuwa wakipanga kuwadhuru raia wa Marekani au maslahi yao katika eneo hilo.

Jenerali Thomas Waldhauser, mkuu wa kikosi cha Africa Command, alisema huko nyuma kwamba itakuwa na “msaada mkubwa” kwa majeshi ya Marekani kuwa na wepesi wa kuamua kufanya mashambulizi na kwa wakati mwafaka.

Serikali ya Somalia mpaka sasa haijatoa tamko lolote kuhusu kauli hiyo ya Marekani.

Laetitia Bader, mtafiti wa shirika la haki za binadamu (Human Rights Watch) anaehusika na Somalia, ametadharisha kuwa lazima mashambulizi hayo yafanyike kwa uangalifu sana, hasa ikizingatiwa hali ya ukame inayoendelea nchini humo.

“Hili litakuwa ndio jambo muhimu wakati huu ambapo tunajua kuwa kuna kuhama kwa raia hivi sasa. Tunazungumzia maelfu ya watu wakihama huku wakijaribu kufikia maeneo yenye miji ilikupata misaada ya dharura kutokana na ukame,” amesema Bader.

XS
SM
MD
LG