Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 19:29

Tinubu ataapishwa licha ya kuwepo kesi kadhaa dhidi yake mahakamani


Rais mteule wa Nigeria Bola Tinubu
Rais mteule wa Nigeria Bola Tinubu

Waziri wa habari wa Nigeria Lai Mohammed amesema rais mteule Bola Tinubu ataapishwa Mei 29 licha ya kuwepo kesi mahakamani kupinga ushindi wake.

Makundi ambayo hayakuridhishwa na matokeo ya uchaguzi wa urais wa februari 25 yanatia wasiwasi kwa serikali ya mpito wakati rais anayemaliza muda wake Muhammadu Buhari akiondoka madarakani rasmi mwezi Mei.

Mohamed alisema “ hakuna msingi” wa katiba ya serikali ya mpito . alisema vyama vya siasa vya upinzani vina haki ya kupinga uchaguzi wa rais mahakamani.

Wagombea wanne wa urais walifungua mashitaka machi 21 kupinga ushindi wa Tinubu kwa madai ya kuenea kwa wizi wa kura na udanganyifu wa kura.

Inachukua takriban miezi minane kwa mahakama kuamua malalamiko ya uchaguzi wa rais. Malalamiko lazima yasikillizwe ndani ya siku 180 tangu siku yalipowasilishwa . mlalamikaji anaweza kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama ya rufaa ndani ya siku 21 tangu tarehe ya uamuzi.

XS
SM
MD
LG