Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 13:32

Timu ya Ferroviario da Beira yapata ushindi wa kwanza BAL


Mchezaji Aten Majok wa US Monastir akipachika pointi dhidi ya CFV Beira huko Dakar Arena Jumapili.(Picha BAL).
Mchezaji Aten Majok wa US Monastir akipachika pointi dhidi ya CFV Beira huko Dakar Arena Jumapili.(Picha BAL).

Timu ya Ferroviario da Beira ya Msumbiji ilipata ushindi wao wa kwanza wa msimu wa pili wa Ligi ya Mpira wa Kikapu barani  Afrika BAL, kwa kuwalaza wenyeji Dakar Universite Club (DUC) 98-92 katika uwanja wa Dakar katika siku ya tatu ya michezo hiyo.

Mchezaji Adama Diakhite alitoa pasi kwa Aboudou na kupachika pointi mbili za kwanza za mchezo kwa DUC.

Wakiwa wamefungana kwa pointi 42 kila mmoja huku zikiwa zimesalia chini ya dakika 4 kipindi cha kwanza kumalizika, Diakhite alimpasia Ali ambaye alichukua mpira na kuupeleka kwa Sane ambaye aliruka juu na kupachika kikapu.

Wakiwa mbele kwa pointi moja, Onwuasor wa Beira alitoa pasi kwa Kennedy ambaye naye alimpasia Perry ambaye alipachika pointi tatu nyavuni na kuwapa uongozi wa pointi nne.

Aboudou wa DUC alimpasia Ali ambaye aliikosa wakati Onwuasor alitoa pasi ya kijanja hadi kwa Orizu aliyepachika pointi nyavuni na kuongeza uongozi wa Beira katika robo ya nne.

Zikiwa zimesalia dakika sita mpira kumalizika, Thierno Niang wa Senegal alikaribia kikapu na kumpasia Diop lakini Munguambe alizuia mpira huo na Beira wakapata pointi mbili upande mwingine.

Jermel Kennedy alitoa asisti kwa William Perry huku timu yake ikiongeza pointi 12 mbele.

Beira iliendelea kusonga mbele huku Munguambe akipachika mpira kwa karibu na kupata pointi mbili naye Perry akipachika pointi tatu zikiwa zimesalia chini ya dakika mbili.

Ali wa DUC alimpasia Diallo ambaye alipachika pointi tatu kupunguza uongozi wa Beira hadi pointi tano.

Thierno Niang alijaribu kupiga pointi tatu nyingine kwa kurusha mara ya mwisho lakini haikutosha kwani Beira tayari waliibuka na ushindi katika kile kilichokuwa ushindani wa karibu kuelekea mwisho wa mchezo huo.

Jermel Kennedy aliiwezesha Beira kwa kumaliza kumaliza na pointi 27 na na rebound 9.

Wakati William Perry alipachika nyavuni pointi 16, Ayade Munguambe pointi 15 na Prince Orizu aliqweka nyavuni pointi 12 na huku Beira wakiboresha rekodi yao ya kanda ya Sahara 1-1 kabla ya pambano lao dhidi ya mabingwa wa Morocco AS Salé .

XS
SM
MD
LG