Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 17:32

Timu ya SLAC ya Guinea yaanza vyema michuano ya BAL


SLAC players and Dakar University Club DUC warming up before their encounter in Dakar Arena Senegal Saturday March 5, 2022 .
SLAC players and Dakar University Club DUC warming up before their encounter in Dakar Arena Senegal Saturday March 5, 2022 .

Timu ya mpira wa kikapu ya Seydou Athletic Club ya Guinea imeanza vyema michuano ya klabu bingwa barani Afrika BAL baada ya kuwabwaga timu mwenyeji Dakar University Club DUC kwa jumla ya pointi 85-70 katika mechi ya ufunguzi katika uwanja wa Dakar Arena Machi 5, 2022.

Mabingwa hao wa Guinea walianza mchezo wakiwa nyuma mpaka mapumziko na kuwashangaza wenyeji DUC katika kota ya tatu baada ya mapumziko wakiongozwa na mchezaji mahiri kutoka Marekani Marcus Crawford aliyejiunga na timu hiyo siku chache zilizopita akipachika jumla ya pointi 30.

Na kuanzia hapo hawakurudi nyuma tena mpaka mwisho wa mchezo. Wenyeji watajilaumu wenyewe walianza vyema na mpaka mapumziko walikuwa wakiongoza kwa pointi 8.

Rais wa Senegal Macky Sall alikuwapo uwanjani akiongoza nchi yake na mashabiki wa DUC katika michuano hiyo ya kihistoria ikiwa ni wenyeji wa kanda ya Sahara lakini bahati haikuwa upande wao.

DUC inabidi washinde michezo yao yote iliyobaki ili kujihakikishia nafasio ya kusonga mbele na wakati huo huo SLAC ya Guinea imejiweka kwenye nafasi nzuri ikiwa itangia katika mechi ya pili ikijiamani zaidi.


Katika mechi hii historia iliandikwa ikiwa ikichezeshwa na refa mwanamke wa kwanza Sara El Chanubi kutoka Misri .

Jumapili ni siku ya pili katika michuano hiyo ambapo timu ya AS Sale ya Morrocco itapambana na wawakilishi wa Afrika mashariki katika michuano ya kanda ya Sahara Rwanda Energy Group-REG.

Michezo yote inaonyeshwa moja kwa moja katika zaidi ya nchi 215.

Washindi wa pili kutoka msimu wa kwanza wa BAL US Monastir na AS Sale wanmejea kwa mara ya pili kwenye ligi hii huku SLAC ya (Guinea), DUC (Senegal), Ferroviario da Beira (Msumbiji) na REG (Rwanda) zote zikicheza mara yao ya kwanza katika ligi hii.

XS
SM
MD
LG