Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Januari 04, 2025 Local time: 15:54

Thailand yawasilisha ombi la kujiunga na BRICS


Watu wakiwa kwenye ukumbi wa soko la hisa la Thailand. Picha ya maktaba
Watu wakiwa kwenye ukumbi wa soko la hisa la Thailand. Picha ya maktaba

Thailand imewasilisha ombi lake la kujiunga na muungano wa mataifa yanayoendelea wa BRICS, unaojumuisha Brazil, Russia, India na Afrika Kusini, ingawa wataalam wanaeleza kuwa na wasi wasi wa iwapo hatua hiyo inafaa.

Nchi wanachama wa BRICS zinataka kuwepo na sarafu mbadala kwa dola ya Marekani inayotumika kwenye mfumo wa kifedha wa kimataifa. Tayari wamebuni taasisi kama Benki Mpya ya Maendeleo, inayoonekana kuwa mshindani wa Benki ya Dunia pamoja na shirika la Kimataifa la Fedha.

Tangu baraza la mawaziri la Thailand kuidhinisha rasimu ya ombi hilo mwishoni mwa Mei, juhudi za kujiunga na BRICS zimeongeza kasi, Waziri mpya wa kigeni wa Thailand, Maris Sangiampongsa, wiki iliopita alirejea nchini, baada ya kuhudhuria mkutano wa BRICS kwenye mji wa Russia wa Nizhny Novgorod.

Msemaji wa wizara hiyo Nikorndej Balankura kupitia taarifa ilioandikwa ameambia VOA kuwa Maris, alikutana na waziri mwenzake wa Russia wakizungumzia BRICS, wakati wa ziara yake. Ameongeza kusema kuwa “Thailand inachukulia BRICS kuwa na jukumu muhimu la kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi wa mataifa ya Kusini mwa dunia, ambao unaendana na maslahi ya kitaifa”.

Forum

XS
SM
MD
LG