Nchi hiyo ya Asia Kusini Mashariki yenye rekodi mbaya ya haki za binadamu katika miaka ya hivi karibuni inatafuta kiti katika Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa, na inaonekana inatumai kuidhinishwa huko kutasaidia ugombea wake wa baadaye mwaka huu, watetezi wa haki za binadamu wanasema.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Thailand imeiambia VOA kwamba lengo ni mkataba huo kuidhinishwa kikamilifu na serikali mjini Bangkok ifikapo Juni 13.
Thailand ilitia saini Mkataba wa Kimataifa wa Ulinzi wa Watu Wote dhidi ya Kutoweka kwa Kulazimishwa (ICPPED) mwaka wa 2012 lakini bado haujaidhinishwa rasmi.
Forum