Thailand ina sifa ya kukumbatia kila mmoja, lakini kwa miongo kadhaa imekuwa na changamoto za kupitisha sheria za ndoa ya jinsia moja.Jamii ya Thailand kwa kawaida hushikilia Imani za kihafidhina, wakati watu wa jamii ya LGBTQ wakidai kubaguliwa katika maisha ya kila siku.
Serikali pamoja na wanaharakati wa haki za kinsia kwa muda mrefu wamekuwa na kibarua kigumu cha kuwashawishi wabunge pamoja na wafanyakazi wa serikali kukumbatia mabadiliko hayo.
Thailand sasa itakuwa nchi ya tatu barani Asia, baada ya Taiwan na Nepal kuruhusu ndoa za jinsia moja. Sheria hiyo ya usawa kwenye ndoa inatoa haki sawa za kisheria za kifedha na kimatibabu kwa kila jinsia, na ilipitishwa kwenye baraza la wawakilishi kabla ya bunge kwenda likizo Aprili, wakati ikipitishwa na wabunge 400 kati ya 415 waliokuwepo.
Forum