Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 29, 2024 Local time: 00:09
VOA Direct Packages

Tanzania: Upinzani unamatumaini CCM itaacha kuwazuia kusema mabadiliko ya sheria yanahitajika


Rais Samia Suluhu Hassan akiwa na mwenyekiti wa Kikosi kazi kilichoratibu maoni ya wadau wa demokrasia nchini, akikabidhiwa ripoti.
Rais Samia Suluhu Hassan akiwa na mwenyekiti wa Kikosi kazi kilichoratibu maoni ya wadau wa demokrasia nchini, akikabidhiwa ripoti.

Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, Chadema kilifanya mkutano wake wa kwanza wa umma hivi karibuni baada ya takriban miaka sita, hii ni kufuatia serikali kuondoa marufuku kwa mikutano kama hiyo.

Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, Chadema kilifanya mkutano wake wa kwanza wa umma hivi karibuni baada ya takriban miaka sita, hii ni kufuatia serikali kuondoa marufuku kwa mikutano kama hiyo.

Licha ya kurejeshwa kwa mikutano kama hiyo, wakosoaji wana mashaka kuwa chama cha CCM ambacho ni cha pili kuwepo madarakani kwa muda mrefu barani Afrika, kitaacha kuwasimamisha wapinzani kusema mabadiliko ya sheria yanahitajika.

Chama cha upinzani cha Chadema kinasherehekea kuondolewa marufuku hiyo ya miaka sita ya kufanya mikutano ya vyama vya siasa, ambapo serikali ilisema itafanyika kwa kuangalia wasi wasi wa usalama.

Naibu katibu mkuu wa Chadema, Benson Kigaila anasema wakati wa marufuku, serikali mara kwa mara iliwalenga wanachama na wafuasi wao, “mazingira ya kisiasa yalikuwa magumu. Watu wengi walikamatwa na tulifunguliwa kesi nyingi ambazo zilikuwa za kubambikiwa. Watu walitiwa ndani na kuteswa, kwa kifupi, kulikuwa na mambo mengi mabaya ambayo yalifanywa,” aliongezea Kigaila.

Makundi ya kutetea haki yanasema rais wa zamani wa Tanzania, marehemu John Magufuli alikuwa akiwakamata wakosoaji wake.

Tangu kifo chake mwaka 2021, Rais Samia Suluhu Hassan ameapa kufungua uwanja wa siasa, ikiwemo marufuku iliyoondolewa mwezi huu kwa mikutano ya vyama vya siasa.

“Wajibu wetu ni kuwalinda ili mkifanya mikutano ya siasa iwe ya amani, mmalize vizuri na muondoke kwa salama. Hilo ndiyo jukumu letu kama serikali. Wajibu wenu kama chama cha siasa ni kufuata sheria na kanuni,” amesema Rais Samia Suluhu Hassan.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, alikaa miezi saba jela kwa shutuma za ugaidi kabla ya upande wa mashtaka mwezi Machi kuachana na kesi hiyo.

Mbowe anasema Rais Samia kuondoa marufuku, na kukutana na wanachama wa upinzani, kumemfanya kuwa na matumaini kuhusu mustakbali wa nchi.

“Nampongeza Rais Samia kwa jinsi alivyokubali mapendekezo yetu kama Chadema wakati wa mikutano yetu. Aliniambia, “Mheshimiwa Mbowe hebu tutafute njia na utamaduni wa kukubaliana kila mmoja.’ Rais alikubali mapendekezo yangu kwa niaba ya wafuasi wote wa Chadema na bado kuna baadhi ya watu ambao wanataka nimshambulie. Kamwe sitafanya hivyo,” alisema Mbowe.

Lakini Chadema na wanaharakati wa haki wanasema rais wa Tanzania anahitaji kusonga mbele na mageuzi ya katiba na sheria, ili haki zisiweze kuchukuliwa tena kwa amri ya kiutendaji.

Anna Henga mkurugenzi mtendai wa Kituo cha Haki za Binadamu, anasema taarifa za viongozi mara nyingi si njia nzuri ya kuongoza katika demokrasia ya nchi yoyote. Kwahiyo, ni kuhakikisha kuwa haki zinaendelea, lazima tuwe na sheria kwasababu kama tukisubiri na kutegemea rais au uamuzi wa chama tawala, hatutasonga mbele kidemokrasia. Kama tukisonga mbele kwa kile ambacho sheria inasema, itatusaidia haki hii iendelee na kutumiwa katika nchi yetu.”

Wakati huo huo, upinzani nchini Tanzania unapanga kuchukua fursa kamili ya kuondolewa marufuku, kwa kuandaa mikutano ya kisiasa nchi nzima.

XS
SM
MD
LG