Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 24, 2024 Local time: 06:47

Upinzani Tanzania umefanya mkutano wao wa kwanza wa hadhara nchini humo


Wafuasi wa chama cha upinzani CHADEMA nchini Tanzania katika mkutano wao wa kwanza wa hadhara kwenye uwanja wa Furahisha Mwanza, Jan. 21, 2023.
Wafuasi wa chama cha upinzani CHADEMA nchini Tanzania katika mkutano wao wa kwanza wa hadhara kwenye uwanja wa Furahisha Mwanza, Jan. 21, 2023.

"Haikuwa rahisi baada ya miaka  saba ya kupiga marufuku mikutano ya kisiasa" mkurugenzi wa mawasiliano na mambo ya nje wa chama cha CHADEMA, John Mrema aliwaambia wafuasi wake waliokuwa wakishangilia

Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania (CHADEMA) kimefanya mkutano wa kwanza wa hadhara tangu kuondolewa kwa marufuku iliyowekwa mwaka 2016 na kuongeza matumaini kwamba serikali imejitolea kuongeza uhuru wa kisiasa katika taifa hilo la Afrika Mashariki.

"Haikuwa rahisi baada ya miaka saba ya kupiga marufuku mikutano ya kisiasa," mkurugenzi wa mawasiliano na mambo ya nje wa chama cha CHADEMA, John Mrema aliwaambia wafuasi wake waliokuwa wakishangilia.

Maelfu ya wafuasi wa CHADEMA walikusanyika katika viwanja vya Furahisha katika jiji la Mwanza lililoko kando ya ziwa Victoria wakiwa wamejipaka rangi ya bluu, nyekundu na nyeupe ya chama hicho.

Rais Samia Suluhu Hassan mwezi Januari 2023 aliondoa marufuku iliyoanzishwa na mtangulizi wake, John Magufuli ambaye alipewa jina la utani la "Bulldozer" kutokana na mtindo wake wa uongozi.

Mabadiliko hayo yaliyofanywa na serikali yanakuja wakati Rais Samia Suluhu Hassan akiwa madarakani kwa miezi 22 akitaka kuondoa baadhi ya sera za Magufuli.

Hatua hiyo ilikaribishwa kwa tahadhari kama faida ya demokrasia na makundi ya kutetea haki za binadamu na vyama vya upinzani nchini Tanzania.

XS
SM
MD
LG