Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 21:30

Tanzania, Kenya zajadili kero 31 za biashara


Rais Uhuru Kenyatta na John Magufuli
Rais Uhuru Kenyatta na John Magufuli

TANZANIA na Kenya zimeanza majadiliano kuhusu vikwazo 31 vya biashara, vinavyosababisha wananchi wa nchi hizo kutoshirikiana vizuri kibiashara.

Hatua hiyo imechukuliwa na pande zote mbili ili kuweka mazingira bora na rafiki ya biashara na uwekezaji katika kukuza uchumi.

Vyanzo vya habari vinasema kuwa moja ya kikwazo katika biashara baina ya nchi hizo ni taratibu katika biashara ya bidhaa ya ngano, ambapo imewataka wasagishaji kutoka nchi zote kuhakikisha wananunua kwanza bidhaa yote ya ngano iliyoko nchini, kabla ya kukimbilia kuagiza kutoka nje ya nchi.

Bidhaa zinazohusika katika vikwazo hivyo ni pamoja na gesi, maziwa na sigara.

Rais John Magufuli na Uhuru Kenyetta walielekeza wizara za biashara kuondoa vikwazo vyote vinavyokwamisha ufanywaji wa biashara baina ya nchi hizo.

Katika mkutano uliowakutanisha wadau mbalimbali wa biashara kutoka Kenya na Tanzania Ijumaa, Katibu Mkuu wa Biashara wa Kenya, Dk Chris Kiptoo alisema serikali hizo zinahitaji kuondoa mara moja vikwazo vyote vya biashara.

Katika mkutano huo, Tanzania iliwasilisha masuala 15 yanayohitaji kujadiliwa na Kenya ikiwasilisha 16 ili kujadili na kufikia mwafaka. Kuhusu ngano alisema unahitajika uwekezaji wa kutosha katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa bidhaa hiyo, lakini pia wamekubaliana kuimarisha kilimo cha zao hilo.

Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Tanzania, Profesa Adolph Mkenda alisema Ijumaa kuwa mkutano huo umelenga kuhitimisha matakwa ya viongozi wakuu wa nchi hizo, wakitaka kuondolewa kwa vikwazo vya biashara.

XS
SM
MD
LG