Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 15:02

Mtandao wa British Airways wadukuliwa


Ndege za shirika la ndege British Airways
Ndege za shirika la ndege British Airways

Takwimu zinazohusiana na maelfu ya wateja wa shirika la ndege la British Airways zimedukuliwa kutoka katika tovuti yake.

Shirika hilo limeeleza Alhamisi jioni kuwa taarifa binafsi na mahesabu ya wateja 380,000 ambao walikuwa wanatumia tovuti ya kampuni hiyo na programu za simu za mikononi kupanga safari zao kati ya Agosti 21 na Septemba 5 zilikuwa zimedukuliwa.

Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa British Airways Alex Cruz amesema kuwa udukuzi huo ulikuwa wa staili ya kipekee, wakiadui, shambulizi la jinai katika tovuti yetu.”

Cruz amesema kuwa British Airways imetumia uwezo wake wote kuwasiliana na wateja wake na kuhakikisha “tunaweza kusaidia kulinda takwimu zao.”

“Tutawalipa fidia wote hao kwa matatizo ya kifedha yaliyo wakabili kutokana na tukio hilo,” amesema Cruz.

Shirika hilo la ndege lilitoa tangazo la kurasa nzima Ijumaa katika magazeti ya Uingereza likisema “Nina omba radhi.”

Shirika la ndege la Uingereza limesema katika tamko lake, “British Airways inaendelea kuwasiliana na wateja walioathirika na tunatoa ushauri kwa mteja yeyote ambaye anaamini ameathirika na tukio hili kuwasiliana na benki zao au watoa huduma ya credit card na kufuata ushauri wanaoupendekeza.

Msemaji wa Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May amesema : “Tunafahamu juu ya ripoti hizi na Kituo cha Taifa cha Usalama wa Mitandao (National Cyber Security Center) na Shirika la Taifa la Jinai (National Crime Agency) wanashughulikia tatizo hili ili kufahamu nini hasa kilichotokea.

XS
SM
MD
LG