Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 26, 2024 Local time: 21:12

Tahadhari mpya yatolewa kuhusu uwezekano wa mashambulizi kwenye michezo ya Olimpiki


Nembo ya Olimpiki kwenye ukuta wa ofisi ya jiji la Paris, Ufaransa.
Nembo ya Olimpiki kwenye ukuta wa ofisi ya jiji la Paris, Ufaransa.

Tahadhari mpya zimetolewa kuhusu uwezekano wa mashambulizi yanayolenga kuvuruga michezo ijayo ya Olimpiki ya majira ya joto mwaka huu  mjini Paris ikiwa pamoja na uwezekano wa njama za kigaidi  kama zile zilizotibuliwa  na maafiwa wa usalama wa Ufarasa wiki iliyopita.

Ripoti iliyotolewa Jumanne na kampuni ya usalama wa mitandao ya Recorded Future, imesema kuwa licha ya uwezekano mkubwa wa mashambulizi ya kimitandao, tishio kubwa kwenye michezo hiyo ni mashambulizi ya moja kwa moja kutoka kwa watu binafsi. Ripoti hiyo imeongeza kusema kwamba “ magaidi na watu wenye misimamo mikali, hasa Islamic State na al-Qaida pamoja na wafuasi wao nchini Ufaransa pamoja na mataifa jirani ya Ulaya, huenda wakaendelea kupanga na kuchochea mashambulizi ya kihalifu yakilenga michezo ya Olimpili ya Paris.”

Tahadhari hiyo imetolewa wakati mamlaka za Ufaransa zikisema kuwa tayari zimezima takriban njama mbili za mashambulizi dhidi ya michezo hiyo. Wiki iliyopita, maafisa wa usalama wa Ufaransa walimkamata kijana wa umri wa miaka 18 , na kumfungulia mashitaka ya kupanga kufanya mashambulizi kwa jina la kundi la kigaidi la Isis, kwenye uwanja wa michezo wa Geoffroy –Guichard mjiji Saint- Etienne.

Forum

XS
SM
MD
LG