Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 16:13

Wachunguzi wa Ufaransa waendelea na upekuzi wa makao makuu ya waandaaji wa michezo ya Paris Olympic


 Matayarisho ya michezo ya Paris Olympic 2024.
Matayarisho ya michezo ya Paris Olympic 2024.

Wachunguzi wa Ufaransa walipekuwa makao makuu ya waandaaji wa michezo ya Paris Olympic Jumanne katika uchunguzi wa vitendo vinavyoshukiwa vya ufisadi, kulingana na ofisi ya kitaifa ya mwendesha mashtaka ya masuala ya fedha.

Kamati ya maandalizi ya Paris imesema katika taarifa yake kuwa upekuzi ulikuwa unaendelea kwenye makao makuu yao katika mji mdogo wa Saint-Denis, na kuwa “Paris 2024 inatoa ushirikiano kwa wachunguzi hao ili kurahisisha kazi yao.” Lakini haikutoa maelezo zaidi.

Paris imekuwa ni mtayarishaji wa michezo kwa mara ya tatu mfululizo ya kipindi cha majira ya joto inashukiwa katika uchunguzi huo unaoongozwa na mamlala ya kupambana na rushwa katika mji mkuu wa Ufaransa.

Madai ya kununua kura yaliyohusishwa na michezo ya Olimpiki ya Rio de Janeiro 2016 na Michezo ya Tokyo 2020 siku za nyuma wanachama kadhaa waliondolewa kutoka katika Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki.

Afisa katika ofisi ya mwendesha mashtaka yanayohusu fedha alisema Jumanne kuwa upekuzi unahusishwa na chunguzi mbili za awali zinazohusiana na Paris Olympics ambazo zilikuwa hazijatangazwa kwa umma.

Afisa huyo alikuwa hajapewa idhini kutajwa jina lake hadharani kulingana na sera ya ofisi ya mwendesha mashtaka.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AP.

Forum

XS
SM
MD
LG