Mann: siku zote nina kadi ndani ya mfuko ambayo inanijulisha leo ni tarehe ngapi. Lazima niandike ninapokula kwasababu mara nyingine naweza kula chakula cha mchana mara tatu kwasababu sikumbuki kama nimeshakula. Madaktari wanasema ubongo wangu unaendelea kupata nafuu na itachukua kiasi cha miaka miwili, lakini chochote ambacho hakijarejea katika kumbukumbu yangu hakitarejea tena.
Salem: Kwa hiyo ulifanyiwa upasuaji November 2008, siyo?
Mann: Ndiyo na kwahiyo maisha yangu yote nitaishi hivi. Kitu ambacho kinanitia khofu sana, ni mawazo kwamba kuna siku nitaamka, na nitakuwa na umri wa miaka 80 na sitakumbuka miaka 40 ya mwisho katika maisha yangu.
Salem: Unakumbuka mara ya kwanza ulipotoka katika upasuaji?
Mann: Najua kwamba siku zote nilikuwa nafikiria nilikuwa San Franscisco.
Salem: Hivyo vitu vinaitwaje, unakumbuka?
Mann: Vikwazo.
Salem: Ndiyo.
Mann: ndiyo, unakumbuka kikwazo kingine ambacho nilikuwa nacho?
Salem: Ulikuwa ukidhani kuwa mfanyakazi mwenzako Barbara, alikuwa mama yako.
Mann: Ndiyo, kweli.
Salem: Ingawaje yeye ni wa rangi tofauti na wewe.
Mann: Ndiyo, kweli.
Salem: Kulikuwa na wakati mmoja ulichanganyikiwa kwa sababu ulidhani tumeachana, nilikuuliza kwanini unadhani unakaa nyumbani kwangu, ukasema kwa vile tunaelewana vizuri.
Mann: (anacheka) ndiyo, samahani kuhusu hilo.
Salem: Hamna neno usijali.
Mann: Na yote uliyokuwa unanifanyia.
Salem: Shukran hilo limeshaondoka.
Mann: Mimi pia nashukuru sana mambo yote mazuri.
Salem: Kwa hiyo, kuna mambo yoyote mazuri ambayo yamekuja kutokana na kupoteza kumbukumbu ambayo unaweza kuyakumbuka.
Mann: Ndiyo, nilikimbia kwenye New York marathon na wewe mpenzi wangu. Moja ya mambo ambayo nilikuomba unisaidie, nisiangalie alama za maili wakati nikikimbia. Na nikikuuliza nimekimbia umbali gani muda wote uniambia kama dakika 10 au 15 (anacheka).
Anaendelea kusema, kwa kweli ilifurahisha sana. Na tulipofika mwisho, mimi na wewe tulikuwa tukikimbia mpaka kwenye mstari wa mwisho, nilianza kulia kwasababu nilikuwa na furaha kubwa. Unajua, nilitumia muda mwingi kujiuguza majeraha na nilihisi vibaya kuhusu mambo ambayo nimepoteza lakini kukimbia marathon inaonyesha bado liko katika mawazo yangu nakumbuka mengi.