Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 22:37

StoryCorps: Mtoto asimulia majukumu ya baba yake


Mkuu wa Familia
Mkuu wa Familia

Kwa miaka 30, John Black alikuwa akifanya kazi kwenye vyumba vya mashine katika shule za umma huko Cincinnati, Jimbo la Ohio, Marekani.

Black alifariki mwaka 2004. Mtoto wake, Samel, kati ya watoto zake 11 – alizungumza na mkewe Edda kumkumbuka baba yake.

StoryCorps: Mtoto asimulia majukumu ya baba yake
please wait

No media source currently available

0:00 0:02:49 0:00

Black alifanya kazi kwa saa nyingi, hasa wakati wa majira ya baridi, kwasababu ilimlazimu kuhakikisha mabomba hayashiki baridi. Chumba cha kupasha moto maji (boiler) kina joto sana.

Edda: je alikuwa akizungumzia kuhusu kazi yake ilivyokuwa?

Black hakuzungumzia hilo. Baba alikuwa anarudi kila siku usiku akiwa amechoka sana na hujitupa tu kitandani. Nakumbuka nilikuwa nachezea misuli yake.

Unajua, kulikuwa na nyakati alikuwa ananiambia nimkande miguu yake. Unajua, wakati huo tulikuwa hatupendi hilo. Alikuwa anafanya kazi saa 16 kwa siku. Akirudi anavua soksi, na anasema nikande miguu, nilikuwa sipendi kwenda karibu na chumba chake, kwa sababu atakuita na kukwambia umkande.

Lakini nikifikiria hivi sasa, pengine mwili wake ulikuwa unamuuma sana, na kukandwa na wanawe ilikuwa ni jambo zuri kwake. Unafahamu, kufanya kazi muda wote huo, hakuwa na muda wa kuzungumza kuhusu mambo mengine. Lazima mambo yote uyafanye yawe sahihi.

Edda: kwa hiyo alikuwa mkali sana?

Black alikuwa mkali. Mara nyingine hakuwa na haja ya kufanya chochote lakini akikuangalia tu, utajua alikuwa anamaanisha nini.

Kwa mfano, nadhani nilipokuwa naumri wa miaka 10, mimi na rafiki yangu lengo letu lilikuwa kupata chupa ya soda na chipsi. Kwahiyo tulikwenda kutafuta chupa, lakini unajua wakati ule lazima ulipie chupa ili uweze kupewa dukani.

Sikuwa na fedha za kutosha kupata soda na chipsi, kwahiyo niliamua kuchukua chupa kutoka dukani na kuziweka kwenye begi langu na halafu nikaenda kuzipeleka dukani nikijifanya kama ni zangu.

Kwa hiyo ghafla nikapata hisia, niliangalia dirishani na kumuona baba yangu akiniangalia, alininyooshea kidole. Nilitoka dukani, na akasema pole pole nenda nyumbani.

Hivyo basi nilikwenda nyumbani na yeye akinifuata nyuma, nilihisi kama niko kwenye maandamano marefu. Nilipofika nyumbani aliniuliza kwanini nilifanya hivyo? nilimwambia nilikuwa nataka senti kumi ili ninunue chipsi. Akaniambia siku nyingine ukitaka pesa mwambie mama yako.

Mpaka baada ya kufariki kwake ndiyo nikagundua kuwa tuliweza kukopa kitu dukani, na kwa hiyo kwenda kuiba pale chupa ya soda kungeweza kuharibu uhusiano mzima.

XS
SM
MD
LG