Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 24, 2024 Local time: 04:13

Moscow: Ajali ya kituo cha treni St. Petersburg inatokana na kujilipua


Mtu awasha mshumaa kuomboleza wale waliouawa na mlipuko St Petersburg, Russia
Mtu awasha mshumaa kuomboleza wale waliouawa na mlipuko St Petersburg, Russia

Wapelelezi wa Russia wamegundua kuwa mzaliwa wa eneo la Kyrgyz- Akbarzhon Dzhalilov kuwa ndiye aliyefanya shambulio la kujilipua la kinyama Jumatatu katika kituo kilichokuwa na watu wengi kwenye mji wa St Petersburg.

Idadi ya wale waliouawa kutokana na mlipuko huo imeongezeka kufikia watu 14, na dazeni za watu kadhaa wengine wamejeruhiwa na wako katika hali mbaya.

Polisi wa Russia wametoa picha ya mshukiwa aliyejilipua Dzhalilov, 22, ambaye wamesema alizaliwa huko Osh na kuwa raia wa Russia mwaka 2011.

“Ndio, kamati ya serikali ya usalama wa taifa imethibisha hilo, kwa kutumia takwimu za mwanzoni, kwamba aliyejilipua alikuwa anaasili ya Kyrgyz, ambaye alichukuwa uraia wa Russia,” amesema Waziri wa Mambo ya Nje wa Kyrgyzstan, Erlan Abdyldaev wakati akikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Sergei Lavrov huko Moscow.

Wapelelezi wa Russia wanasema Dzhalilov aliweka bomu la pili katika kituo kingine cha treni katika mji wa St Petersburg ambalo polisi waliligundua na kuzuia lisiripuke. Hakuna kikundi mpaka sasa kilichodai kuhusika na shambulizi hilo lakini vyombo vya serikali vinachunguza uwezekano wa kuwepo mahusiano na kikundi cha Islamic State.

Viongozi wa ulimwengu kutoka China mpaka Ulaya hadi Brazil wametuma rambirambi zao juu ya tukio hilo la mauaji. Rais Donald Trump ameongea kwa simu na Rais wa Russia Vladimir Putin na kumhakikishia kumsaidia ipasavyo katika kukabiliana na shambulizi hilo.

XS
SM
MD
LG