Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 18:41

Mfalme wa Jordan kuwasilisha Kwa Trump mkakati wa amani


Mfalme Abdullah II
Mfalme Abdullah II

Mfalme wa Jordan Abdullah II ataweza kuwasilisha makubaliano ya nchi za Kiarabu kuhusu amani ya Mashariki ya kati wakati anakutana na Rais Donald Trump katika Ikulu ya White House Jumatano.

Makubaliano hayo yalifikiwa katika mkutano wa hivi karibuni ulioandaliwa na mfalme ambao uliibua upya pendekezo la Waarabu kuitambua Israeli na hivyo kubadilishana na Israeli kwa kuwepo taifa la Wapalestina.

Kuna wanaojiuliza iwapo kuibuka upya kwa mpango huo wa Waarabu, na baadhi ya kauli za Trump zenye kuelezea nia ya kufikia makubaliano, kunaonyesha dalili za kuanza mazungumzo kati ya Waisraeli na Wapalestina? Huu ndio mtizamo hivi sasa.

Kitu gani kiko katika meza ya mazungumzo?

Katika mkutano wao wa mwaka wiki iliopita, viongozi wa Kiarabu waliibua upya pendekezo lililotolewa kwa Isreali 2002- ambapo dazeni ya nchi za Kiislamu na Kiarabu zilikubali kuitambua Israeli kwa kubadilishana nao na kuundwa kwa taifa la Palestina katika Ukingo wa Magharibi na Jerusalem mashariki.

Hata hivyo Israeli imesita, kati ya mambo mengine, katika upeo wa matarajio ya kuondoka kutoka katika ardhi hizo ilizozikamata mwaka 1967 na bila mafanikio kujaribu kulizungumzia upya pendekezo hilo la awali.

Kwa kauli ya mkutano huo ambayo inasaidia pendekezo lake, Mfalme wa Jordan ataweza kumwambia Trump kwamba viongozi wa Kiarabu wanania kufikia kile waziri wa mambo ya nje wa Jordan, Ayman Safadi, alichokieleza kuwa “ni suluhisho la kihistoria kati ya Israeli na ulimwengu mzima wa Kiarabu.”

Lakini mfalme huyo atakuwa na baadhi ya vivutio vitavyowezesha kupatikana amani ya eneo lakini pamoja na kutoa tahadhari.

Jordan inatoa hoja kuwa mgogoro wa Israeli na Palestina wenye miongo mingi unabakia kuwa ni mzizi wa vurugu katika eneo hilo na kuwa kama utaachiwa kuendelea, utadhoofisha lengo la uongozi wa Trump Mashariki ya Kati la kuidhibiti Iran na kuwatokomeza kikundi chenye siasa kali cha Islamic State.

XS
SM
MD
LG