Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 09:55

Marekani yasitisha msaada kwa shirika la UN


Rais Donald Trump
Rais Donald Trump

Uongozi wa Trump unasimamisha ruzuku inayotolewa na Marekani kwenye shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya watu (UNFPA), ukilituhumu kwa kusaidia utoaji mimba wa kulazimishwa au ufungaji kizazi bila hiari.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imewatumia barua Kamati ya Mambo ya Nje ya Baraza la Seneti Jumatatu ikisema itazuia dola milioni 32.5 katika bajeti yake ya 2017 kwenda UNFPA.

Barua hiyo imesema Shirika hilo, linalojulikana kama UNFPA, linafanya kazi na Tume ya Afya ya Taifa na Mpango wa Uzazi ya China, ambayo inatekeleza “sera ya watoto wawili” ya Beijing ambayo inawazuia familia za Kichina idadi ya watoto wanaotaka kuwa nao.

Wizara ya Mambo ya Nje inasema itahamisha pesa kwenda katika mpango wake wa ndani wa afya duniani.

Katika tamko lake, UNFPA imesema inasikitishwa na uamuzi huo uliofanywa na uongozi wa Trump, ambao inasema umefikiwa kwa “madai yasiosahihi” kwamba inasaidia utoaji mimba wa kulazimishwa au kufunga kizazi bila hiari nchini China.

Jukumu la UNFPA limejikita katika uzazi wa mpango wenye kufuata utaratibu, pamoja na afya ya mama na mtoto.

Uamuzi huo ni wapili kufanywa na uongozi wa Trump kuzuia fedha za Marekani kwenda katika vikundi vya kimataifa juu ya suala linalofungamana na utoaji mimba.

Rais Donald Trump amerudisha kile kinachoitwa “global gag rule”, kanuni ambayo inakataza kufadhili vikundi visivyo vya kiserikali ambavyo vinashiriki au vinatoa maelekezo katika utoaji mimba.

Sera hizi kwa kawaida zinabadilika ikitegemea chama gani kinamamlaka Ikulu ya White House.

Warepublikan, kama ilivyokuwa wakati wa Rais mstaafu George W. Bush, inaonyesha walikuwa na msimamo sawa na Trump, ambapo ilikuja kubadilishwa na Mdemokrat Bill Clinton na Barack Obama.

Lakini uamuzi wa Rais Trump unazidi kudhihirika katika pendekezo lake la bajeti inayotaka punguzo kubwa katika bajeti ya diplomasia na misaada ya nje ya Wizara ya Mambo ya Nje, ikiwepo misaada kwa ajili ya Umoja wa Mataifa kwa pamoja.

XS
SM
MD
LG