Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 21, 2024 Local time: 16:05

Sitisho la mapigano la Gaza lafika mwisho wakati kukiwa na matumaini ya kuongezwa kwa muda


Avihai Brodutch akiwakumbatia watoto wake Oria Brodutch, 4, na Ofri Brodutch, 10, pamoja na mke wake Hagar Brodutch baada ya kuungana nao tena Israel, November 26 kufuatia kuachiliwa kwao na Hamas.
Avihai Brodutch akiwakumbatia watoto wake Oria Brodutch, 4, na Ofri Brodutch, 10, pamoja na mke wake Hagar Brodutch baada ya kuungana nao tena Israel, November 26 kufuatia kuachiliwa kwao na Hamas.

Israel na Hamas Jumatatu wameingia kwenye siku ya nne na ya mwisho ya sitisho la muda la mapigano, wakati kukiwa na matumaini ya Israel kuwaachilia wafungwa zaidi wa kipalestina.

Hamas kwa upande wao wanatarajiwa kuwaachilia mateka zaidi, wakati kukiwa na shinikizo la kuongezwa muda wa sitisho hilo. Hamas ilikuwa imeashiria kuongezwa kwa muda huo wakati waziri mkuu wa Israel Benjamini Netanyahu akirudia kusema Jumapili kwamba Israel ilikuwa tayari kuongeza muda huo, iwapo Hamas watawaachilia mateka 10 zaidi kwa siku.

Makubaliano ya kwanza yaliyoanza kufanya kazi baada ya wiki 6 za mapigano, yaliihusisha Hamas kuwaachilia jumla ya mateka 50, huku Israel ikiwaachilia wafungwa 150 wa kipalestina, wakati mapigano yakiwa yamesitishwa kwa muda.

Umoja wa Mataifa umesema Jumapili kwamba jumla ya waisraeli 39, wapalestina 117 na raia wa kigeni 19 wameachiliwa ndani ya kipindi hicho. Marekani, Misri na Qatar ni miongoni mwa mataifa yanayoshinikiza kuongezwa kwa muda huo baada ya kuwa mstari wa mbele kufanikisha sitisho la sasa la mapigano.

Marekani, Misri na Qatar ni kati ya nchi zinazo hamasisha kuongezwa muda wa baada ya kushirikiana kufanikisha kupatikana kwa sitisho la mapigano la siku nne.

“Hilo ndiyo lengo langu, hilo ndiyo lengo letu, kuendeleza utulivu huu kuwa zaidi ya kesho ili tuweze kuendelea kuona mateka zaidi wanaachiliwa na misaada ya kibinadamu zaidi inafikishwa kwa wale wenye shida huko Gaza,” Rais wa Marekani Joe Biden aliwaambia waandishi wa habari Jumapili.

Biden pia alifurahia kuachiliwa kwa mtoto wa kike wa miaka minne kimarekani mwenye asili ya Israel mwenye miaka minne ambaye wazazi wake waliuawa mwezi Oktoba 7 katika shambulizi la Hamas dhidi ya Israel.

Msichana huyo, Abigail Edan, ni kati ya Waisraeli 14 na raia watatu wa kigeni waliokabidhiwa kwa Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu katika siku ya tatu ya Hamas kuwaachilia mateka kwa mabadilishano na Wapalestina walioachiliwa huru na Israel ambao walikuwa wamefungwa kwa makosa mbalimbali.

Katika taarifa yake White House ilisema kuwa Biden na Netanyahu walizungumza kuhusu kuachiliwa mateka kwa njia ya simu Jumapili, na kuwa walijadili kusitishwa kwa mapigano na kuongezwa kwa msaada zaidi ya kibinadamu kuingia Ukanda wa Gaza.

Kusitishwa kwa muda kwa mapigano ni sitisho la kwanza katika mgogoro huo tangu Hamas, katika shambulizi la kushitukiza dhidi ya Israel Oktoba 7, lililouwa watu 1,200 na kuwateka takriban watu 240. Israel kwa upande wake iliahidi kuwatokomeza Hamas na kufanya mashambulizi ya anga na ardhini huko Gaza ambapo maafisa wa Palestina wanasema yameuwa zaidi ya watu 14,000, asilimia 40 vifo hivyo ni vya watoto.

Huko Barcelona, Mkuu wa sera za mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell amesema usitishaji wa mapigano huo wa siku nne ni “hatua muhimu ya kwanza,” lakini alisema hatua zaidi zinahitajika ili “kuleta afueni kwa hali mbaya iliyoko Gaza na kutafuta suluhu ya mgogoro huo unaoendelea.

Baadhi ya taarifa katika habari hii inatokana na mashirika ya habari ya Associated Press, Agence France-Presse na Reuters.

Forum

XS
SM
MD
LG