Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 21, 2024 Local time: 16:07

Israel inasema wanamgambo wa Hamas wamewaachilia huru mateka wengine 17


Abigail Edan mwenye miaka minne ni mmoja wa mateka walioachiwa huru na wanamgambo wa Hamas.
Abigail Edan mwenye miaka minne ni mmoja wa mateka walioachiwa huru na wanamgambo wa Hamas.

Msichana Abigail Edan alikuwa miongoni mwa Wa-Israeli 14 na raia watatu wa kigeni waliokabidhiwa kwa Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu katika siku ya tatu ambayo Hamas imewaachia mateka kwa mabadilishano na Israel iwaachilie raia wa Palestina ambao wako jela kwa makosa mbalimbali

Israel imesema Jumapili kuwa wanamgambo wa Hamas wamewaachilia huru mateka wengine 17 waliokuwa wakishikiliwa Gaza, akiwemo msichana wa miaka minne, raia wa Marekani ambaye Rais wa Marekani Joe Biden alisema alishuhudia wazazi wake wakiuawa na Hamas wakati wa shambulio lao huko kusini mwa Israel wiki saba zilizopita.

Msichana Abigail Edan, alikuwa miongoni mwa Wa-Israeli 14 na raia watatu wa kigeni waliokabidhiwa kwa Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu katika siku ya tatu ambayo Hamas imewaachia mateka kwa mabadilishano na Israel iwaachilie raia wa Palestina ambao wako jela kwa makosa mbalimbali. Biden alisema, “kile alichokipitia huyu hakiwezi kufikirika.”

Kiongozi wa Marekani alizungumza na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, baadaye kuhusu kuachiliwa huru kwa mateka hao wakati wa mpango wa Israel wa kusitisha mapigano kwa siku nne katika mashambulizi yake dhidi ya wanamgambo wa Hamas huko Ukanda wa Gaza, eneo dogo kwenye bahari ya Mediterania.

Nembo ya White House
Nembo ya White House

White House imesema katika taarifa yake kwamba Biden na Netanyahu pia walijadili kusitisha mapigano na kuongeza misaada inayohitajika sana ya kibinadamu kuingia Gaza. “Waziri Mkuu wa Israel alimshukuru Rais wa Marekani kwa juhudi zake bila kuchoka kusaidia kufanikisha na kutekeleza kikamilifu makubaliano haya”, ilisema taarifa hiyo.

“Viongozi hao wawili walikubaliana kwamba kazi bado haijakamilika na wataendelea kufanya kazi ili kufanikisha kuwaachiliwa huru kwa mateka wote.

Forum

XS
SM
MD
LG