Maafisa wa afya wanasema vikosi vya Israel vinavyoendesha operesheni zake huko Ukingo wa Magharibi vimewaua Wapalestina wasiopungua wanane, akiwemo mwanamgambo mmoja katika kipindi cha saa 24.
Ghasia zinazoongezeka huko Ukingo wa Magharibi zinakuja wakati sitisho tete la mapigano huko Ukanda wa Gaza kati ya Israel na Hamas limeingia siku yake ya tatu.
Wizara ya Afya ya Palestina imesema Wapalestina watano wameuawa katika ngome ya wanamgambo wa Jenin, huku wengine watatu waliuawa katika maeneo tofauti ya Ukingo wa Magharibi tangu Jumamosi asubuhi.
Jeshi la Israel limesema vikosi vya Israel viliwaua Wa-palestina watano, katika shambulizi la bunduki wakati wa uvamizi wa kuwakamata wakimbizi wa Jenin. Moja ya madai hayo yalidaiwa na kundi la wanamgambo kama mwanachama.
Forum