Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Novemba 18, 2024 Local time: 08:34

Trump azungumzia upigaji vita ufadhili wa ugaidi na viongozi wa GCC


Rais Donald Trump akutana na Mfalme wa Bahrain Hamad bin Isa Al Khalifa, huko Riyadh, Saudi Arabia, Mei 21, 2017.
Rais Donald Trump akutana na Mfalme wa Bahrain Hamad bin Isa Al Khalifa, huko Riyadh, Saudi Arabia, Mei 21, 2017.

Ziara ya Rais Donald Trump siku ya pili nchini Saudi Arabia imefungamana na mikutano na viongozi mbalimbali wa eneo hilo la Mashariki ya Kati na anashiriki katika mazungumzo ya Baraza la Ushirikiano wa Ghuba ya Uajemi (GCC).

Wakati wa mkutano wa GCC, wanachama watabadilishana nyaraka juu ya kupambana na ufadhili wa ugaidi.

“Ni matarajio yetu tutaweza kufukia azma ya pamoja kuacha kuvifadhili vikundi vya kigaidi ambapo Hazina ya Marekani itakuwa ikifuatilia kwa karibu na wizara husika katika nchi ambazo ni washirika wetu

…Kitu cha kipekee katika hatua hii ni kwamba kila mmoja wao ni wenye kusaini makubaliano jinsi watavyokuwa wanawajibika na watawashtaki wale wanaofadhili ugaidi, wakiwemo watu binafsi,” Naibu Mshauri wa Usalama wa Taifa Dina amewaabia waandishi.

Pamoja na Marekani, washiriki wa mkutano huo wa GCC ni Bahrain, Kuwait, Oman, Qatar, Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu.

Ikulu ya White House hawakutoa tamko mara moja juu ya mkataba huo.

Trump pamoja na viongozi wa GCC walishuhudia naibu mrithi wa Ufalme Mohammed bin Nayef na Waziri wa Mambo ya Nje Rex Tillerson wakibadilishana nyaraka za makubaliano.

Trump, ambaye yuko kwenye ziara yake ya kwanza ya kigeni amekubali kufanya mipango mingine ya ziara mpya.

Rais amesema Jumapili kwamba atakubali mualiko uliotolewa na Rais wa Misri Abdel Fattah el-Sissi kutembelea Misri.

Trump amesema ziara hiyo itafanyika muda sio mrefu katika siku za usoni.

“Tumekuwa kwa hakika pamoja na Sissi katika mambo mengi, mambo ambayo ni chanya… ametusaidia sana katika kuachiwa huru mfanyakazi wa kujitolea Aya (Hijazi), rais alisema huku akiongezea kuwa, “ Tunayo baadhi ya mambo muhimu tunayo zungumzia kwa pamoja na Misri. Na umefanya kazi nzuri katika mazingira magumu yenye majaribio na usalama unaelekea kuimarika kabisa.”

Al-Sissi amejibu (kupitia mkalimani): “Itakuwa ni heshima kubwa iwapo utatutembelea Misri… Egypt inaendelea kuimarika vizuri kwa msaada tunaopata kutoka Marekani. Tunatarajia kuwa na ushirikiano zaidi kwa ajili ya utulivu na usalama wa eneo hili la dunia. …Wewe unahadhi ya kipekee katika kufanya vitu ambavyo vinaonekana kuwa haviwezekani.”

XS
SM
MD
LG