Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Januari 26, 2025 Local time: 09:41

Trump, Mfalme Salman wasaini mkataba wa ulinzi wa $110-bilioni


Rais Trump na Mfalme Salman wakisaini mkataba wa ulinzi.
Rais Trump na Mfalme Salman wakisaini mkataba wa ulinzi.

Rais Donald Trump na Mfalme wa Saudi Arabia Salman bin Abdulaziz wamesaini mkataba wa dola za Marekani bilioni 110 kuboresha uwezo wa kijeshi wa Saudi Arabia, huko Riyadh Jumamosi.

"Makubaliano haya ya kuendelea kuwaimarisha katika vifaa vya ulinzi na huduma ambazo ni mkakati wa ulinzi wa muda mrefu wa Saudi Arabia na nchi nyingine mashariki ya kati ili kukabiliana na vitisho vya Iran."

"Wakati huo huo makusudio ya Saudi Arabia ni kuongeza uwezo wake katika kupambana na operesheni za ugaidi katika eneo hilo, ili kuwapunguzia mzigo mzito jeshi la Marekani katika kufanya operesheni hizo," tamko la ikulu ya White House limesema.

Ikulu ya White House imeongeza kusema kuwa mkataba huo utaongeza fursa kwa makampuni ya Marekani katika kufanya biashara Mashariki ya Kati na kusaidia kutoa ajira mpya "kwa maelfu ya watu katika secta ya ulinzi ya Marekani.

Pia katika makubaliano hayo kuna ahadi ya dola bilioni 6 ya kuziunda helikopter za kivita Lockedheed Martin Blackhawk nchini Saudi Arabia, ambazo zitawezesha fursa za ajira 450 nchini Saudi Arabia.

XS
SM
MD
LG