Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 20:25

Watu wanne wauawa katika shambulizi Uingereza


Watu walioumia wakiondoshwa katika sehemu ya tukio Uingereza
Watu walioumia wakiondoshwa katika sehemu ya tukio Uingereza

Sio chini ya watu wanne akiwemo mtu aliyemshambulia afisa wa polisi, wamethibitishwa kuwa wamekufa katika shambulizi karibu na Bunge la Uingereza ambalo vyombo vya dola vinalichunguza kama tukio la kigaidi.

“Japo kuwa tuko wazi katika kujua sababu iliyopelekea shambulizi hili, uchunguzi kamili katika kuzuia ugaidi unafanywa,” Kamanda BJ Harrington ameuambia mkutano wa waandishi Jumatano nchini Uingereza.

Pia wanafanya msako kuhakikisha kwamba hakuna watu wengine wanaopanga mashambulizi, japokuwa maafisa wa polisi wameeleza kuwa shambulio hilo lilifanywa na mtu mmoja peke yake.

Jengo la Bunge la Uingereza, London limefungwa na watu wanazuiwa kupita, kuingia au kutoka baada ya mshambuliaji huyo kumpiga kisu afisa wa polisi kabla ya kupigwa risasi na maafisa wengine waliokuwa katika viwanja vya bunge.

Askari aliye jeruhiwa baadae alikufa kwa majeraha. Sio chini ya watu wawili waliuawa na wanane kujeruhiwa wakati gari lililopo wagonga watu kadhaa karibu na daraja la Westminster.

Afisa wa ngazi ya juu wa Polisi ameiambia VOA kuwa wanaamini kulikuwa na mshambuliaji mmoja tu katika kile kilichoonekana kama ni shambulizi lilopangwa katikahatua tatu tofauti.

Askari wa stesheni ya Metro, London wamesema wanalichukulia tukio hilo kuwa ni la kigaidi mpaka pale watapopata taarifa zaidi, wakiongeza kuwa bado hali ni tata na wamewasihi watu kukaa mbali na eneo hilo.

Maafisa wa usalama wamesema mtu aliyekuwa na kisu alimchoma nacho afisa wa polisi kabla ya kuuawa na askari.

Kiongozi wa Bunge la Uingereza David Lidington amesema kulikuwa na taarifa ya matukio mengine ya uvunjifu wa amani ndani ya jengo hilo.

Taarifa za walioshuhudia na picha mwanzoni zilionyesha watu wawili wakitokwa na damu nyingi karibu na daraja la Westminster, ambapo polisi ya Uingereza imesema maafisa wake walikabiliana na “tukio lililohusisha silaha.”

Watu walioshuhudia tukio hilo baadae waliripoti kuwa gari moja iliwagonga watu kadhaa katika daraja hilo. Picha pia zinaonyesha baadhi ya walioumia katika daraja hilo. Lakini mpaka sasa haijulikani idadi ya wahanga wa tukio hilo.

XS
SM
MD
LG