Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 05:50

Shambulio la anga la Israel ladaiwa kuuwa watu 14


Moto ukiwaka katikati ya Gaza, wakati wa vita Septemba 11, 2024. Picha na REUTERS/Amir Cohe
Moto ukiwaka katikati ya Gaza, wakati wa vita Septemba 11, 2024. Picha na REUTERS/Amir Cohe

Shambulio la anga la Israel lauwa takribani watu 14 wakiwemo watoto wawili, wakati lilipopiga shule ya Umoja wa Mataifa iliyokuwa hifadhi ya familia za Wapalestina waliopoteza makazi katikati ya Gaza siku ya Jumatato, maafisa wa hospitali wamesema.

Jeshi la Israel limesema shambuluo hilo lilikuwa likiwalenga wanamgambo wa Hamas waliokuwa wakipanga shambulio kutoka ndani ya shule hiyo.

Maafisa kutoka hopitali ya Awda huko Nuseirat wamesema wamepokea miili ya watu 10 waliokuwa wamekufa kutokana na shambuluo hilo, na wengine wanne walikuwa wamepelekwa katika hopitali ya Deir al-Balah.

Tariban mwanamke mmoja na watoto wawili ni miongoni mwa waliouawa, na takribani watu 18 wamejeruhiwa katika shambulio hilo, maafisa wa hopitali wamesema.

Mmoja wa watoto hao alikuwa binti wa Momin Selmi, mwanachama wa shirika la ulinzi wa raia, ambalo linafanya kazi ya kuokoa watu waliojeruhiwa na kuopoa miili ya watu baada ya mashambulizi, taarifa ya shirika hilo imesema.

Forum

XS
SM
MD
LG