Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 14:51

Sessions apitishwa na Kamati ya Sheria ya Baraza la Seneti


Seneta Jeff Sessions
Seneta Jeff Sessions

Kamati ya Sheria ya Baraza la Seneti imempitisha Seneta Jeff Sessions wa Republikan kuwa Mwanasheria Mkuu Jumatano.

Siku mbili baada ya kuibuka utata unaoendelea juu ya amri ya Rais Donald Trump kuzuia wasafiri wanaotaka kuja Marekani kutoka nchi saba za kiislamu, ambayo ilipelekea kaimu mwanasheria mkuu kufukuzwa kazi kwa sababu ya utovu wa nidhamu.

Uteuzi wa Sessions sasa utakwenda kwenye Baraza la Seneti lote ambako kuna matarajio makubwa kwamba atathibitishwa katika wadhifa huo kwani chama cha Republikan kina wingi wa kura 52.

Kura ya kamati imekuja wakati maseneta wademokrat wameazimia kuchelewesha kupitishwa kwa wateule wa Trump, akiwemo mteule wa nafasi ya Hazina, Steve Mnuchin na mteule wa kuongoza Wizara ya Afya na Huduma za Kibinadamu, Tom Price.

Hata hivyo sasa Sessions atasubiri kupigiwa kura na Baraza la Seneti katika siku zijazo.

Kama ilivyokuwa ikitarajiwa kuwa warepublikan na wademokrat wangegawanyika katika uteuzi huo ulio na utata, lakini alipitishwa kwa kura 11-9. Kamati hiyo ilipiga kura katika misingi ya chama.

Wakati warepublikan wakiwa tayari kumpitisha seneta mwenzao wa siku nyingi katika baraza hilo kuwa ndio msimamizi wa juu wa sheria nchini, wademokrat wameendelea kudadisi iwapo Sessions atakuwa anafanya maamuzi ya kujitegemea bila ya kuingiliwa kati na Rais Trump.

XS
SM
MD
LG