Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 14:54

Trump amemteuwa Neil Gorsuch kuwa jaji wa mahakama kuu


Rais Trump akipeana mkono na jaji mteule Neil Gorsuch.
Rais Trump akipeana mkono na jaji mteule Neil Gorsuch.

Rais Donald Trump amemteua jaji wa serikali kuu katika jimbo la Colorado, Neil Gorsuch kuwa jaji wa mahakama ya kuu ya Marekani.

Rais Trump alisimama mbele ya kamera za televisheni kwenye Ikulu ya Marekani jumanne usiku kumwelezea Gorsuch, akimuita mtu ambaye nchi inamuhitaji sana na anasema kwamba ujuzi na elimu yake haiwezi kuzusha mvutano wowote. Rais Trump alisema wakati wa kampeni yake, aliwaahidi wapiga kura kwamba atamtafuta jaji bora zaidi kwa nchi.

Alisema barua ya kazi na historia ya elimu ya Gorsuch ikiwemo shahada kutoka chuo kikuu cha Columbia na chuo cha sheria cha Harvard ni nzuri. Aliwataka wademokrat na warepublikan katika baraza la seneti ambao lazima wamuidhinishe, waungane pamoja kwa mara nyingine kwa manufaa ya nchi.

XS
SM
MD
LG