Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 22:37

Serikali yakamata tani 20 za korosho katika ghala binafsi


Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga,
Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga,

Vyombo vya dola nchini Tanzania vimekamata tani 20 za korosho kutoka ghala la Olam linalomilikiwa na mtu binafsi mkoani Mtwara.

Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga, amesema Jumamosi kuwa korosho hizo zilikabidhiwa katika Chama cha Msingi cha Mnyawi kwa lengo la kuchanganywa kinyemela na zile zinazopelekwa kwenye maghala makuu, limeripoti gazeti la Mtanzania.

“Jana (juzi) tulikamata tani 20 zilizokuwa zimepenyezwa katika vyama vya msingi, tusingependa lijirudie hivyo, wananchi wawe makini kuhakikisha korosho zinazoletwa katika vyama vya msingi ni zile za Watanzania ili korosho yetu peke yake iendelee kununuliwa na Serikali,” amesema Hasunga.

Amesema korosho zitakazokamatwa kutoka nje ya nchi au kuingizwa kinyemela kwenye vyama vya msingi zitataifishwa na wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari hicho, Jumanne wiki hii, tani nyingine tisa zilikamatwa katika eneo la Newala baada ya kuingizwa kinyemela toka nchini Msumbiji.

Pia imeripotiwa kuwa siku ya Alhamisi iliyopita yalikamatwa magunia 152 ya korosho katika Wilaya ya Nanyumbu yalioingizwa kutoka Msumbiji.

XS
SM
MD
LG