Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 05:26

Serikali Tanzania yatoa agizo jipya kupambana na ulanguzi wa madini


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

Serikali ya Tanzania imeziamuru kampuni zote zinazochimba madini nchini kufungua vituo vya mauzo ndani ya nchi, vitakavyo simamiwa na serikali, ikiwa ni mkakati wa kukabiliana na biashara haramu ya madini ya thamani ya juu hasa dhahabu, inayozalishwa nchini humo.

Vyanzo vya habari nchini humo vimeripoti kuwa vituo hivyo vitatoa fursa kwa wachimbaji madini wadogo wadogo kupata soko maalum linalosimamiwa kisheria, ili waweze kuuza madini yao.

Kwa sasa, wachimba madini wadogowadogo wanapata changamoto kadhaa kupata mawakala walioidhinishwa na sheria, ambao idadi kubwa wanapatikana katika mji wa Dar-es-salaam na miji mingine mikubwa.

Taarifa kutoka ofisi ya Waziri Mkuu inasema kwamba kituo cha kwanza kwa ajili ya kuuza madini, kinachomilikiwa na kampuni ya AngloGold kutoka Afrika Kusini, kimefunguliwa kaskazini magharibi mwa nchi, katika mji wa Geita.

Tanzania inashikilia nafasi ya nne kwa utajiri wa madini barani Afrika, baada ya Afrika kusini, Ghana, na Mali, na hupata takriban dola bilioni 1.5 kutoka kwa uuzaji wa madini nje ya nchi.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG