Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 05:40

Senegal yazuia huduma za intaneti kudhibiti ujumbe wa chuki unaosambazwa


Ousmane Sonko
Ousmane Sonko

Senegal imezuia huduma za internet kuanzia Jumatatu kutokana na kuenea kwa ujumbe wa chuki katika mitandao ya kijamii, waziri wa mawasiliano ameeleza katika taarifa yake.

Haya yanakuja baada ya kiongozi wa upinzania Ousmane Sonko kushitakiwa jumamosi kwa kupanga uasi, njama za mapinduzi, njama za kihalifu na makosa mengine.

Mwendesha mashtaka wa umma wa Senegal jumamosi alitangaza kwamba makosa saba zaidi dhidi ya kiongozi wa kisiasa na mkosoaji mkubwa wa rais Macky Sall ambaye anakabiliwa na msusuru wa matatizo ya kisheria anayodai kuwa yanalenga kumuondoa katika uwanja wa kisiasa.

Katika Mkutano na waandishi wa habari Jumapili kwenye mji mkuu wa Dakar, mawakili wa Sonko walisema mamlaka hawakuheshimu haki zake.

Sonko alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela Juni mosi kutokana na kesi ya rushwa.

Forum

XS
SM
MD
LG