Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 19:38

Mwanachama wa upinzani Senegal ameshtakiwa kwa kumkejeli Rais Sall


Sheria na mkondo wake
Sheria na mkondo wake

Mashtaka dhidi ya Birame Souleye Diop, mwanachama mwandamizi wa chama cha kisiasa cha Pastef, na muungano wa upinzani wa Yewwi Askan Wi yanahusishwa na kauli ya kudhalilisha aliyoitoa wiki iliyopita kuhusu nia ya kisiasa ya Rais Macky Sall.

Mwanasiasa mmoja wa upinzani nchini Senegal ameshtakiwa kwa kosa la kejeli dhidi ya rais wa nchi hiyo, wakili wake amesema katika kesi kuhusu matamshi aliyoyatoa hivi karibuni kuhusu Rais Macky Sall.

Mashtaka dhidi ya Birame Souleye Diop, mwanachama mwandamizi wa chama cha kisiasa cha Pastef, na muungano wa upinzani wa Yewwi Askan Wi yanahusishwa na kauli ya kudhalilisha aliyoitoa wiki iliyopita kuhusu nia ya kisiasa ya Rais Macky Sall.

Sall hapo Julai 3 alitangaza kwamba hatogombea muhula wa tatu madarakani wenye utata, katika uchaguzi wa mwaka ujao, na kumaliza miezi kadhaa ya hali ya sintofahamu.

Katika mkutano na waandishi wa habari siku iliyofuata, Diop alieleza kwamba rais anaweza kutoa tangazo na kuligeuza. Alitoa tahadhari kwa wagombea wa siku zijazo katika chama cha Sall. Epuka kula nyumbani kwake, epuka kunywa maji yake, ana uwezo wa kukuwekea sumu na kusema, Kwa kuwa hatuna mgombea tena, ninarudi kuwania kiti hicho, Diop alisema.

Diop ambaye baadaye aliomba msamaha kwa matamshi hayo alishtakiwa Jumanne kwa kufanya vitendo vinavyoweza kuhatarisha amani ya umma na uhalifu dhidi ya Rais wa Jamhuri, wakili wake Moussa Sarr, aliliambia shirika la habari la AFP.

Forum

XS
SM
MD
LG