“Ninafahari kubwa kwa washindi wetu,” amesema Mkurugenzi wa VOA, Amanda Bennett. “Mafanikio haya yanaonyesha upeo wa vipaji na umahiri ulionyeshwa na waandishi wetu ambao wanafanya kazi kwa bidi kila siku, katika mazingira hatarishi kwa maisha yao, kuuletea ulimwengu wa wafuasi wetu habari mpya, za ukweli na zenye mfuto.”
Makala maalum ya VOA yenye jina la Boko Haram: Safari ya Uovu (Boko Haram: Journey from Evil) ambayo inaonyesha uchambuzi wa kina wa Boko Haram, kikundi chenye msimamo mkali ambacho kimeitia hasara Nigeria , ilichukua nafasi ya kwanza katika filamu ya kundi la masuala ya kimataifa.
Makala hiyo inadhihirisha ulimwengu uliojificha wenye madhila ya utesaji na mauaji iliyoandaliwa katika masaa 18 ya video za siri za Boko Haram ambazo zilitafutwa na VOA, na zinatathmini misingi ya Boko Haram, hatua zinazochukuliwa na serikali ya Nigeria, na simulizi zenye kuhamasisha za Watu shujaa wa Nigeria wanao hatarisha maisha yao ili kurejesha hali yao kawaida.
Timu hiyo ilioshinda inajumuisha Mzalishaji Mtendaji, Beth Mendelson, Mkurugenzi Mtendaji wa matangazo kwa njia ya simu, Idhaa ya VOA Hausa, Ibrahim Ahmed, Mhariri msimamizi habari za uchunguzi wa kituo cha Habari cha VOA, Tom Detzel na juhudi ya pamoja ya watu wengi wabunifu kutoka nchi mbalimbali duniani.
Pamoja na tuzo hiyo, Makala za Televisheni Nje ya Barabara Kuu (Off The Highway) ya Kituo cha Habari cha VOA, zinazoangaza sauti za watu wa vijijini na mji mdogo Marekani, kimeshinda medali ya shaba kwa fungu la habari zinazoripotiwa zinazoendelea kutokea.
Makala hizo Nje ya Barabara Kuu inawapa fursa wafuatiliaji wa VOA nchini Marekani taswira mbalimbali na ufahamu wa maeneo ya Marekani ambayo mara nyingi hayaripotiwi kama ilivyo kwa maeneo ya mijini katika pwani ya mashariki na magharibi.