Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 22:08

Saudi Arabia yakanusha ilijaribu kudukua simu ya mmiliki wa Amazon


Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Saudia Faisal bin Farhan Al-Saud
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Saudia Faisal bin Farhan Al-Saud

Saudi Arabia imekanusha ripoti inayodai kuwa ilijaribu kudukua simu ya muanzilishi wa kampuni ya Amazon, Jeff Bezos.

Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Saudi Arabia Faisal Bin Farhan al Saud amesema kwenye mkutano wa Davos kuwa madai hayo ni upuuzi mtupu.

Tamko hilo limekuja baada ya ubalozi wa Saudia mjini Washington kutoa ujumbe kama huo kwenye ukurasa wake wa Tweeter.

Siku Jumatano maafisa wawili wa Umoja wa Mataifa watawasilisha ripoti inayoeleza kwamba kuna ushahidi wa kutosha unaodhihirisha kwamba Saudi Arabia ilidukua simu ya Bezos.

Ripoti hiyo inaeleza kwamba simu yake huenda ilidukuliwa kupitia ujumbe wa video iliyotumwa kupitia ukurasa wa WhatsApp wa mwana wa mfalme mrithi wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman.

Ripoti hiyo inatazamiwa kuharibu zaidi uhusiano kati ya mtu tajiri kabisa duniani na utawala wa kifalme baada ya mauaji ya Jamal Khashoggi aliyekuwa anafanya kazi na Gazeti la Washington Post linalomilikiwa na Bezos.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG