Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Novemba 21, 2024 Local time: 23:00

Samsung yasema simu yake mpya ya Galaxy S23 itavutia mamilioni ya wateja


Simu mpya za Samsung Galaxy S23
Simu mpya za Samsung Galaxy S23

Kampuni ya Korea Kusini ya kutengeneza vifaa vya kielektroniki, Samsung, imesema ina matumaini makubwa kwamba simu zake za mkononi za kizazi kipya, zitapata umaarufu zaidi mwaka huu kote duniani.

Kampuni hiyo inaelezea imani hiyo ikisema kuwa imeimarisha teknolojia yake kwa kiwango kikubwa, katika kutengeneza simu zake mpya aina ya S23, S23 Plus na S23 Ultra, zilizozinduliwa hivi karibuni.

Wakati kampuni ya Apple ikiendelea kutawala katika soko la simu nchini Marekani, Kimataifa, Samsung imeendelea kuonyesha umahiri wake.

Uzinduzi wa simu zake mpya aina ya S23, S23 Plus na S23 Ultra ulifanyika hivi karibuni katika ukumbi wa kihistoria wa Masonic mjini San Fransico katika jimbo la California hapa Marekani.

Samsung S23 Ultra mpya inayoonyesha kile ambacho kamera yake inaweza kufanya.

Drew Blackard, ni makamu Rais wa ubora wa bidhaa za kampuni ya Samsung

"Mwaka huu, simu za Galaxy S23 na S23 Plus, zinaiga muundo huu wa kipekee, na kuleta taswira ya kuvutia kwa simu zote. Kuanzia muundo, hadi nguvu zake, uwezo wa Ultra unadhihiriswha na kamera yetu ambayo ni bora zaidi, " alisema.

Huu ndio mtindo unaotumia teknolojia ya juu zaidi katika mfululizo wa simu zake za Galaxy.

Kampuni hiyo kubwa ya teknolojia ya Korea inajivunia uwezo wa simu zake mpya, wa kupiga picha bora zaidi. Ultra kwa mfano, inakuja na kamera ya mega pixel 200, kumaanisha kwamba picha zina mwonekano wa juu sana na rangi zaidi.

Hata katika hali ya chini ya mwanga, Samsung inaahidi picha bora, hata kwa watengeneza filamu.

Vifaa vyote vilivyozinduliwa vinaendeshwa na chipsi za Qualcomm Snapdragon 8 Gen 2, chipset ya kizazi kipya yenye uwezo ulioboreshwa wa AI.

Laini mpya ya simu za Galaxy S23 ilionyeshwa, ikiwa kamili na kamera mpya na zilizoboreshwa na utendakazi kuboreshwa.

Pia uwezo wake wa kuhifadhi data umeongezwa, na kukifanya kifaa bora hata kwa watengenezaji wa video za kuweka kwenye mitandao ya kijamii, akama anavyoelezea James Kitto, makamu rais wa kampuni ya Samsung, wa uboreshaji wa simu za mkononi Uingereza na Ireland.

"Unaweza pia kuwa mtengenezaji wa maudhui. Unaweza kuhariri video popote ulipo. Unaweza kutengeneza video za ubora wa hali ya juu, za mfumo wa 8K, na unaweza kucheza michezo ya video. Unaweza kucheza michezo ya simu ya mkononi bora zaidi kuliko wakati mwingine wowote. Ni simu yenye nguvu sana. Hii ndiyo bidhaa yenye nguvu zaidi ambayo tumewahi kutengeneza," alisema.

S23 Ultra itagharimu $1,199 itakapouzwa mnamo Februari 17, bei sawa na S22 Ultra ya mwaka jana.

Simu za Samsung Galaxy S23 na S23 Plus hazina nguvu kama Ultra, lakini zinakuja na uboreshaji wa kamera na betri, na pia bei zake ni nafuu, zikiuzwa kwa dola $799 na $999 mtawalia.

Pia kulikuwa na toleo la Ultra la laptop ya Galaxy Book. Kifaa, ambacho kinalenga wabunifu na wataalamu wengine wa biashara. Bei yake inaanzia dola $2,399.

Hii ilikuwa hafla ya kwanza ya uzinduzi wa ana kwa ana, iliyofanywa na kampuni ya Samsung tangu kuanza kwa janga la COVID-19 karibu miaka mitatu iliyopita.

XS
SM
MD
LG