Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 05:25

Sakata la Mafuta Kenya: Raila aishauri serikali iwashirikishe wananchi


Raila Odinga
Raila Odinga

Serikali imeshauriwa kuanzisha mazungumzo ya kitaifa kujadili kuongezeka kwa deni ili kuweza kufikia ufumbuzi juu ya sakata la ushuru wa asilimia 16 uliowekwa kwenye bidhaa za mafuta nchini Kenya.

Mwandishi wa idhaa ya Kiswahili VOA anaripoti kuwa deni hilo hivi sasa limefikia takriban shilingi trilioni tano ambazo ni sawa na dola za Marekani bilioni 49.

Akitoa ushauri huo wa serikali kufanya mazungumzo Jumatatu, Kiongozi wa upinzani Raila Odinga amesema kuwa mikopo hii kutoka mataifa ya kigeni ni mzigo mkubwa kwa raia wa Kenya.

Wakati huohuo mjadala unaendelea Kenya, wananchi wakinong’onezana kuhusu deni la nchi kutoka mataifa ya Kigeni, hususan Uchina na iwapo Kenya inajiingiza katika mtego wa madeni ya China.

Akiwa kwenye mkutano kati ya viongozi wa bara la Afrika na
China jijini Beijing, Rais Uhuru Kenyatta alifanya mashauriano na mwenzake Xi Jingping juu ya njia bora ya kudumisha mahusiano yake na taifa hilo la Asia.

Aidha, katika mashauriano hayo kati yake na China, serikali ya Kenya imeeleza kupata ufanisi wa aina yake; kuweza kuyashawishi makampuni binafsi kuja kuwekeza mabilioni ya fedha nchini Kenya.

Imesema uwekezaji huo hasa ni katika ujenzi wa barabara kuu yenye kilomita thelathini kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta hadi Westlands jijini Nairobi na vile ujenzi wa kituo cha uchumi kiitwacho Dongo Kundi Special Industrial Economic Zone mjini Mombasa.

Pia, mkataba umesainiwa wa kujenga barabara kuu yenye kilomita 143 kuanzia Modogashe-Habaswein-Samatar Mandera na Elwak-Rhamu kwa shilingi bilioni kumi na tano.

Na japo kuwa Rais Xi Jinping alieleza Kenya pamoja na mataifa mengine ya Afrika kuwa uwekezaji wake haufungamani na masharti yoyote, kuwekeza huku kumeonekana na baadhi ya wachambuzi kuwa chambo au mtego wa kuingiza Kenya katika madeni zaidi.

Mwaka 2017, Uchina imeonekana kuwa mkopeshaji mkuu wa Kenya kwa asilimia 72% kwa zaidi ya shilingi bilioni 520 na kufuatwa na Japan shilingi bilioni 80, Ufaransa bilioni 60 na Ujerumani bilioni 30.Kwa mujibu wa takwimu za hazina ya Kitaifa Kenya.

XS
SM
MD
LG