Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 13:58

Safaricom Kenya kuendelea kuitumia Huawei kutekeleza mradi wa 5G


Kampuni ya simu ya Safaricom ya Kenya imesema kampuni yake inatafakari kuipatia kandarasi kampuni kuu ya mawasiliano ya China ya Huawei kutekeleza mradi wake wa mtandao wa 5G mwaka 2020.

Serikali ya Marekani inataka Huawei, ambayo ni mojawapo ya makampuni yanayo fanya kazi na Safaricom pamoja na Nokia kufungiwa kuingia katika baadhi ya masoko ya biashara ya mawasiliano ikiwa ni pamoja na ujenzi wa mtandao wa 5G huko Uingereza na Ulaya.

Akizungumza na shirika la habari la Reuters juu ya msimamo huo wa Marekani, Mkurugenzi Mtendaji wa Safaricom Michale Joseph alisema wataitumia Huawei katika kujenga mtambo wa mtandao wa 5G ambao inauwezo wa kuunganisha vifaa mbalimbali vya kielectroniki mbali na simu na kompyuta na kupakua na kupandisha sauti, picha, video kwa spidi kubwa zaidi.

Mkurugenzi huyo amesema : "Ni kitu gani tutakacho,kifanya kuhusiana na msimamo wa Marekani kuhusu utumiaji Huawei? Hatuna suala hilo hapa Afrika. Sidhani Marekani itatuambia kile kenya inabidi kufanya au kutofanya . Ni uhusiano tofauti kati ya Marekani na Afrika.

Wachambuzi wanasema kujihusisha kwa Huawei katika mfumo wa 5G wa Safaricom utaweza kuzusha matatizo katika mazungumzo juu ya biashara huru kati ya Marekani na Kenya yaliyotangazwa wiki ilyiopita hapa mjini Washingotn.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG