Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 06, 2024 Local time: 20:53

Safari kuelekea kwenye mabaki ya Titanic yaanza tena baada ya ajali ya mwaka jana


Picha maalum iliochukuliwa chini ya bahari ikionyesha mabaki ya meli ya Titanic.
Picha maalum iliochukuliwa chini ya bahari ikionyesha mabaki ya meli ya Titanic.

Kampuni inayomiliki haki za kuokoa meli ya Titanic inaanza safari yake ya kwanza , hilo likifanyika mwaka mmoja baada ya mkasa wa chombo kilichokuwa kimebeba watu kutoka kwa kampuni nyingine kuuwa watu watano.

RMS Titanic Inc, yenye makao yake kwenye jimbo la Georgia ina haki za kuokoa meli hiyo iliozama kwenye bahari ya Atlantic Kaskazini 1912. Safari imeanza Ijumaa kuanzia kwenye mji wa Providence, Rhode Island, ya mwisho ikiwa ilifanyika 2010. S

afari hiyo inafanyika wakati jamii ya watafiti wa chini ya bahari wakiwa wangali wameshtushwa na ajali ya chombo kilichoporomoka kikielekea kwenye meli hiyo Juni mwaka uliopita. Wote waliokuwa kwenye chombo hicho walikufa akiwemo Paul Henri Nargoelet, ambaye alikuwa mkurugenzi mkuu wa utafiti kwenye kampuni ya RMS.

Mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo Jessica Sanders amesema kuwa sasa ndiyo watafanya hata zaidi licha ya kifo cha Nargoelet, ambaye wengi kwenye kampuni hiyo walimuita Mr Titanic.

Forum

XS
SM
MD
LG